
WATU watatu
wamekufa katika matukio mawili tofauti jijini Dar es Salaam, wakiwemo wawili
walioteketea kwa moto baada ya nyumba kuungua, huku mwingine ambaye ni msichana
wa miaka 16 akifa kwa kujinyonga. Kwa mujibu wa Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa
Ilala, Marietha Minangi, aliyejinyonga ni Milika Kusenha.
Alisema binti
huyo alikutwa akiwa amejinyonga juzi saa 1:00 asubuhi maeneo ya Vingunguti
Mtakuja, wilaya ya Ilala.
Alijinyonga kwa
kutumia kitenge na mtandio alivyoviunganisha na kufunga kwenye kenchi chumbani
kwa mwanamke aliyetajwa kwa jina la Naomi Milimo (24), aliyekuwa anaishi nae.
Hata hivyo sababu za kujinyonga hazijafahamika, maiti imehifadhiwa katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Katika tukio
jingine, moto uliozuka ghafla katika nyumba inayomilikiwa na Ramadhani Kambenga
yenye vyumba vinne, uliteketeza kabisa vyumba hivyo pamoja na kusababisha vifo
vya watu wawili.
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Temeke, Engelbert Kiondo alisema moto huo ulizuka juzi saa 5:00
usiku katika eneo la Keko Mwanga na vyumba viwili vya mpangaji aitwaye Michael
David (28) pamoja na mali zote, pia kumuunguza mtoto wake aitwaye Johnson
Michael (6) na rafiki yake aliyetajwa kwa jina moja la Abuu anayekadiriwa kuwa
na umri kati ya miaka 30 na 35.
Kutokana na
miundombinu mibovu ya barabara magari ya zimamoto yalishindwa kufika katika eneo
la tukio, moto huo ulizimwa na wananchi wa eneo hilo kwa kutumia mchanga na
maji. Chanzo cha moto huo inasadikiwa kuwa ni hitilafu ya umeme.
Maiti
zimehifadhiwa hospitali ya Temeke, upelelezi unaendelea. Katika tukio la tatu,
moto ulizuka ghafla katika nyumba ya Komba Dominick (68) mkazi wa Mtoni Mtongani
na kuteketeza mali zenye thamani ya Sh milioni 26.
Kamanda Kiondo
alisema tukio la moto huo lilitokea juzi saa 7:00 mchana Mtoni Mtongani, ambapo
uliteketeza ghala la kuhifadhia makasha matupu mali ya mpangaji Lameck Anania
(55).
Pia moto huo
ulishika nyumba ya jirani aitwaye Mahamudu Chibango (53) na kuunguza nyaya za
umeme pamoja na vyumba viwili.
Moto ulizimwa na
kikosi cha zimamoto na uokoaji cha jiji kwa kushirikiana na wananchi wa eneo
hilo na chanzo cha moto huo bado hakijafahamika.
Post a Comment