Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Bi. Suzzan Kaganda Akiongea na waandishi wa Habari hawapo pichani, Katika ukumbi wa Mikutano wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma Kuhusia na ajali iliyotokea katika kijiji cha Fufu, Kata ya Fufu, Wilaya ya Chamwino, ambapo takribani magari matano (5) yaliyokuwa kwenye msafara wa Mwenge wa Uhuru, yakitokea Wilaya ya Dodoma kuelekea kwenye makabidhiano Wilaya ya Mpwapwa, ambapo Watu wapatao tisa (9) walijeruhiwa katika ajali hiyo
Mkuu
wa Kikosi cha Usalama Barabarani Wilaya ya Dodoma, Mrakibu wa Jeshi la
Polisi Bw. Bonventure Nsokolo Akikagua moja ya gari iliyoharibika katika
ajali iliyotokea katika kijiji cha Fufu, Kata ya Fufu, Wilaya ya
Chamwino, ambapo takribani magari matano (5) yaliyokuwa kwenye msafara
wa Mwenge wa Uhuru, yakitokea Wilaya ya Dodoma kuelekea kwenye
makabidhiano Wilaya ya Mpwapwa
Baadhi
ya washiriki walikuwa katika msafara wa kwenda kukabidhi mwenge kutoka
wilaya ya Dodoma mjini na kuukabidhi katika wilaya ya Mpwapwa
wakiangalia moja ya magari yaliyoharibika baada ya kutokea ajali hiyo
Gari namba DFP.7178 TOYOTA LAND CRUISER (AMBULANCE) ambayo ni mali ya
Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma. Picha na Luppy Kung’alo wa Jeshi la Polisi Dodoma
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
TAARIFA YA POLISI MKOA WA DODOMA KWA VYOMBO VYA HABARI TAREHE 20/08/2013
Mnamo
tarehe 20/08/2013 majira ya 08.45 hrs. huko katika kijiji cha Fufu,
Kata ya Fufu, Wilaya ya Chamwino, takribani magari matano (5) yaliyokuwa
kwenye msafara wa Mwenge wa Uhuru, yakitokea Wilaya ya Dodoma kuelekea
kwenye makabidhiano Wilaya ya Mpwapwa, moja ya magari yaliyokua kwenye
msafara huo lilikutana na tuta huku dereva wake akishika ‘brake’ ghafla
na kusababisha magari yaliyokuwa nyuma yake kugonga gari la mbele kwa
kila moja lililokuwa likitimka kutokana na vumbi kubwa lililokuwa
likifuka wakati wa msafara huo kufuatia matengenezo ya barabara Dodoma –
Iringa yanayoendelea
Katika ajali hiyo magari yaliyoathirika ni kama ifatavyo:-
1. STK 3007 TOYOTA LAND CRUISER
2. STK 3357 TOYOTA LAND CURISER yote ni mali ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa Katibu Tawala [M] Dodoma.
3. SM 5835 TOYOTA LAND CRUISER mali ya Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma
4. DFP.7178 TOYOTA LAND CRUISER (AMBULANCE) nayo ikiwa ni mali ya Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma.
5. T.627 BFJ TOYOTA LAND CRUISER mali ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma
6. STK 4983 TOYOTA LAND CRUISER HARD TOP Mali ya Wizara ya Kilimo.
Watu
wapatao tisa (9) walijeruhiwa katika ajali hiyo, kati yao wanne (4)
wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa Dodoma na watano (5) walipatiwa
matibabu na kuruhusuiwa kurudi nyumbani.
Majeruhi waliolazwa ni kama ifuatavyo:-
1. JUMA S/O ALLY @ SIMAI, Miaka 32, Mpemba, Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa, Mkazi wa Kusini Unguja.
2. CHARLES S/O MAMBA, Mgogo, Miaka 50, Mkazi wa Ipagala, Diwani wa Kata ya Ipagala
3. DATIVA D/O KIMOLO, Miaka 46, Mrangi, Afisa Mifugo, Manispaa ya Dodoma, Mkazi wa Mailimbili.
4. AMINA D/O MGENI, Miaka 36, Muuguzi Kituo cha Afya Makole, Mkazi wa Area ‘C’ Manispaa ya Dodoma.
Majeruhi waliotibiwa na kuruhusiwa kurudi makwao ni kama ifuatavyo:-
1. JACKLINE D/O MAGOTI, Miaka 39, Mjita, Muuguzi Kituo cha Afya Makole, Mkazi wa Area C Manispaa ya Dodoma
2. RICHARD S/O MAHELELA, Miaka 51, Mgogo, Mwenyekiti wa Mtaa wa Ipagala, Mkazi wa Ipagala Manispaa ya Dodoma
3. JUMANNE
S/O NGEDE, Miaka 58, Mrangi, Diwani Kata ya Chamwino/ Naibu Meya wa
Manispaa ya Dodoma, Mkazi wa Chamwino Manispaa ya Dodoma.
4. ZAITUNI D/O VARINOI, Miaka 43, Mkazi wa Mbwanga, Manispaa ya Dodoma.
Jeshi
la Polisi Mkoa wa Dodoma linatoa wito kwa madereva na watumiaji wa
barabara hususan zilizopo kwenye matengenezo wanapokuwa katika misafara,
wanapaswa kuwa makini na wapeane nafasi kati ya gari moja hadi jingine
ili kuepusha madhara yanayoweza kuepukika.
[Suzzan. S. Kaganda - ACP]
Kny: KAMANDA WA POLISI [M] DODOMA
Post a Comment