Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Silima(wa pili kulia) akikata utepe kuashilia uzinduzi rasmi wa Duty free shop ya Gereza Kuu
Karanga, Moshi jana Agosti 23, 2013(wa kwanza kulia) ni Kamishna
Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja. Kamishna
Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja akitoa maelezo mafupi
kwa Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Pereira
Silima kabla ya kumkaribisha kuzindua rasmi Duty free shop ya Gereza
Kuu Karanga, Moshi jana Agosti 23, 2013. Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Silima( kulia)
akiangalia jiwe la msingi mara baada ya uzinduzi rasmi wa Duty free shop
ya Gereza Kuu Karanga, Moshi jana Agosti 23, 2013(kushoto) ni
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja. Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Silima( katikati) akiwa
katika picha ya pamoja na Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John
Casmir Minja(wa pili kushoto) pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali
wa Mkoa wa Kilimanjaro na Wakurugenzi wa
Transit Military Shop mara baada ya uzinduzi rasmi.
Kikundi cha kwaya ya Kina Mama wa Kambi ya Gereza Kuu Karanga Moshi wakitumbuiza wakati wa hafla ya Uzinduzi rasmi wa Duty free shop ya Gereza Kuu Karanga mbele ya mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Silima(hayupo pichani). (Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza)
Transit Military Shop mara baada ya uzinduzi rasmi.
Kikundi cha kwaya ya Kina Mama wa Kambi ya Gereza Kuu Karanga Moshi wakitumbuiza wakati wa hafla ya Uzinduzi rasmi wa Duty free shop ya Gereza Kuu Karanga mbele ya mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Silima(hayupo pichani). (Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza)
………………………………………………………………………
Na; Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza, Moshi
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhe. Pereira Silima amepongeza kasi ya Utendaji kazi wa Kamishna
Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja pamoja na Uongozi wote
wa Jeshi la Magereza Nchini kwa kutekeleza kwa mafanikio makubwa mpango
wa Serikali wa kuwasogezea huduma za bidhaa muhimu na zenye manufaa
Maafisa, askari Magereza na familia zao katika maeneo yao ya kazi
hususani huduma za “Duty free shops”. Mhe. Pereira Silima ameyasema hayo jana wakati wa uzinduzi
rasmi wa Duty free shop ya Gereza Kuu Karanga, Moshi jana Agosti 23,
2013 katika Viwanja vya Gereza Kuu Karanga Moshi ambapo baadhi ya
Viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Kilimanjaro walihudhuria hafla hiyo.
Aliongeza kuwa Serikali iliidhinisha utaratibu wa Maafisa na
askari wa Majeshi ya Polisi na Magereza kusogezewa huduma za kuwapatia
bidhaa muhimu katika maeneo yao kwa gharama nafuu. “Lengo la Mpango huu ni kuhakikisha kuwa ustawi wa maisha ya
Maafisa na Askari wa Majeshi haya kwa kuwapatia bidhaa zenye bei nafuu
ili kuwapunguzia ukali wa maisha” alisema Mhe. Silima.
Aidha, Mhe. Silima amewaasa Maafisa na askari watakaotumia huduma husika kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu pamoja na maadili ya uendeshaji wa maduka hayo ili kuhakikisha kuwa adhima ya Serikali ya kuwapunguzia makali ya maisha Maafisa, askari pamoja na familia zao wananufaika ipasavyo na si vinginevyo.
Awali akimkaribisha Mgeni rasmi,Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja alisema kuwa Jeshi la Magereza kwa kushirikiana na Transit Military Shop LTD limeazimia kusambaza huduma za Duty Free Shop nchi nzima kwa ajili ya kutoa huduma kwa Maafisa na askari.
Kamishna Jenerali Minja alimhakikishia Mgeni rasmi kuwa maduka hayo yataendeshwa kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na taza Duty Free Shop na akasema kuwa hata sita kuchukua hatua kali za kinidhamu kwa Maafisa na askari watakao kwenye kinyume na uendeshaji wa huduma hizo.
Hivi sasa Jeshi la Magereza limefanikiwa kuzindua jumla ya Duty Free Shops tatu(03) katika ya Ukonga, Dar es Salaam, Gereza Isanga Dodoma na Gereza Kuu Karanga, Moshi na tayari maandalizi ya uzinduzi katika Mikoa ya Morogoro, Mwanza, na Mbeya yatakamilika hivi karibuni.
Post a Comment