Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho, Fred Shoo, aliwaonesha waandishi wa habari shehena ya pamba hiyo wakati ikipakuliwa katika kinu na kufanyiwa uchunguzi na wataalamu wa zao hilo mbele ya mkulima mwenye mali hiyo.
Shoo alisema kwa kawaida pamba inapochanganywa na maji na kufungwa katika mafurushi au marobota huoza na kutoa harufu mbaya kutokana na joto na mkandamizo ghalani au kwenye gari, jambo lililofanya kampuni yake kubaini dosari hiyo kabla ya kuinunua.
Alitoa wito kwa Bodi ya Pamba nchini, wakuu wa mikoa, wilaya, watendaji wa kata na vijiji kuwaelimisha wakulima wa zao hilo vijijini ili kuepukana na hasara wanayoweza kuipata endapo pamba yao itakataliwa sokoni na kurudishwa.
Naye Lukelesha alikiri kuwapo kwa takataka na maji katika shehena yake ya pamba na kuelekeza lawama kwa familia yake kwa uzembe uliosababisha kuharibika kwa pamba yake.
Timu ya wataalamu wa kinu cha kuchambua pamba wakiongozwa na Meneja wa kiwanda, Robert Ndallahwa, walidai kuwa uchakachuaji wa zao hilo hufanywa kwa makusudi ili kuongeza uzito kwa lengo la kupata faida zaidi, jambo linaloharibu ubora wa zao hilo.
TANZANIA DAIMA
Post a Comment