
"MIILI ya askari wawili wa Kituo cha Polisi cha mjini Namanyere wilayani Nkasi mkoani Rukwa, Konstebo John Mkoma (26) mwenye nambari H1 na Benjamin Justine (27) mwenye nambari G 9696 imesafirishwa kwenda makwao kwa maziko.
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda alithibitisha leo kuwa, tayari miili hiyo
ya askari hao vijana imesafirishwa jana jioni kwenda vijijini kwako kwa mazikom
.
Aliongeza kuwa
mwili wa Kontebo Mkoma umesafirishwa kwenda kijijini Msangano wilaya mpya ya
Momba mkoani Mbeya ambapo mwili wa Konstebo Benjamin umesafirishwa kwenda
kijijini Hedaru mkoani Kilimanjaro kwa maziko .
Kwa mujibu wa
Mwaruanda askari hao walikufa baada ya kugongwa na gari linalodaiwa kuwa katika
mwendo kasi Alhamisi wiki hii saa mbili za usiku usiku mjini Namanyere katika
barabara ya kutokea Soko Kuu kwenda katika Kituo hicho cha Polisi kikazi
.
Alibainisha kuwa
ajali hiyo ya barabara ilihusisha pikipiki yenye namba za usajili T 903 DUP mali
ya Mkoma aliyekuwa amempakia mwenzake, na gari aina ya Toyota Hiace lenye namba
za usajili T 875 CJC, mali ya Kaimu Mhandisi wa Maji wa Wilaya ya Nkasi, Simon
Salala (31) ambaye ndiye aliyekuwa akiendesha gari hilo.
Akielezea tuko
hilo, Mwaruanda alisema usiku huo polisi walikuwa wakielekea kazini, lakini
ghafla waligongwa na Salala aliyekimbia na gari hadi nyumbani kwake na yeye
mwenyewe kwenda kujificha,lakini baada ya msako alikamatwa na sasa na sasa
anashikiliwa na jeshi polisi.
Post a Comment