
Alisema
hadi sasa wameingia ubia na kampuni ya kutengeneza mabasi ya Eicher pamoja na
wasambazaji wa mabasi ya kampuni hiyo ya Africarries kwa ajili ya kufanikisha
uwekezaji huo.
"Tumeanza
mpango mkubwa wa uwekezaji na tumeingia ubia na Eicher na Africarries ambapo
ifikapo Juni, 2014 mabasi 2,000 yatakuwa yamefika nchini na ifikapo Septemba na
Oktoba mabasi mengine 100 itakuwa yamefika na hayo ni mbali na yale 2,000,"
alisema Kisena.
Alisema
katika awamu ya kwanza walianza na mabasi 30 na sasa mabasi mengine 40 yapo
tayari na yataanza kutoa huduma hivyo kufanya jumla ya mabasi ya UDA kufikia 70.
Aliongeza kuwa ifikapo mwaka 2017 UDA itakuwa na mabasi yanayotoa huduma ya
usafiri yapatayo 7,000 na mipango ya kufanikisha uwekezaji huo inaenda vizuri.
"Uwekezaji
huu utakuwa na manufaa kwa wakazi wa Dar es Salaam...uwekezaji wa UDA nia yake
ni kugusa maisha ya wananchi, tutaleta mabasi ambayo yatasaidia wananchi wa rika
zote, wanawake na wanafunzi," alisema Kisena na kuongeza kuwa;
"Hii sio mipango wa
ubabaishaji v i n g i n e v y o h a t a h a w a wasingekuwepo (maofisa wa
Africarriers." Alisema uwekezaji huo wa mabasi 2,000 utakapoanza zitazalishwa
ajira za watu 8,000, hivyo watu wengi wataweza kupata kazi," alisema na kuongeza
kuwa;"Nauli za mabasi yetu zitakuwa hazipandi hovyo hovyo, kwani sisi tupo kwa
ajili ya wananchi na hata kama kutakuwa na hali ya kupanda kwa mafuta, nauli
haitakuba inabadilika mara kwa mara.
Alifafanua kuwa ununuzi
wa mabasi 2,000 ni maandalizi ya kuingia na kutoa huduma kupitia Mradi wa Mabasi
yaendayo Kasi Dar es Salaam (DART), kwani mabasi yanayoagizwa na UDA ni yale
yanayokidhi masharti yanayotakiwa ikiwa ni pamoja na kuwa na milango miwili ya
kutumiwa na abiria.
Aliongeza kuwa sehemu
kubwa ya faida itaelekezwa kwa jamii hasa kwa upande wa elimu na sekta ya afya.
Alibainisha kwamba baada ya UDA kuwa imara hisa zake zitaingizwa kwenye Soko la
Hisa Dar es Salaam (DSE ) ili watu wapate fursa ya kununua hisa hizo baada ya
kutengeneza minzania yake mwakani.
Wakati huo huo, Kisena
alisema wao wapo tayari kununua hisa ndani ya UDA iwapo itafanyika hivyo. "Na
sisi tumesikia kwenye vyombo vya habari kuwa Jiji la Dar es Salaam litauza hisa
zake, endapo watafanya hivyo sisi tutakuwa tayari kuzinunua, lakini hatukatazi
mtu mwingine kujitokeza kuzinunua,"alisisitiza
Post a Comment