Jeshi
la Polisi Nchini linatoa shukrani kwa wananchi wote wakiwemo waandishi
wa habari, viongozi wa dini, wanasiasa, makampuni binafsi ya ulinzi kwa
ushirikiano mkubwa wanaoutoa kwa njia mbalimbali katika kuhakikisha
kwamba nchi yetu ya Tanzania inakuwa salama na raia wote wanaishi kwa
amani na utulivu bila hofu ya uhalifu na wahalifu.
Katika kipindi hiki cha kuelekea
sikukuu ya Eid-El-Fitr, Jeshi la Polisi linatoa tahadhari kwa wananchi
wote kuwa makini na kuchukua hatua stahiki na za haraka kwa kutoa
taarifa pindi wanapoona viashiria vyovyote vya uhalifu katika maeneo
wanamoishi na sehemu mbalimbali zikiwemo maeneo ya biashara.
Ikumbukwe kuwa, wananchi wenye
imani ya kiislam na hata madhehebu mengine hutumia muda huo kwenda
kuabudu pamoja na muendelezo wa sherehe hizo kwenye maeneo mbalimbali ya
starehe. Uzoefu unaonyesha kuwa baadhi ya watu hutumia kipindi hicho
cha sikukuu kama mwanya wa kufanya matukio ya uhalifu kutokana na
mikusanyiko hiyo ya watu. Jeshi la Polisi limejipanga vizuri kwa
kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama katika kuhakikisha
kwamba, wananchi wote wanasherekea sikukuu hiyo kwa amani na utulivu,
pasipo vitendo ama viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani.
Ulinzi umeimarishwa kwenye maeneo
yote ya kuabudia, fukwe za bahari, sehemu za starehe na maeneo mengine
yote ambayo yatakuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu.
Aidha, wale wote ambao watakuwa
wakitumia barabara, wanatakiwa kuwa makini kwa kuzingatia sheria za
usalama barabarani na hasa kwa madereva wa magari na pikipiki kuepuka
kwenda mwendo kasi na kutumia vilevi wawapo kazini.
Katika kuhakikisha usalama kwenye kumbi za starehe, wamiliki wa kumbi hizo wazingatie uhalali na matumizi ya kumbi zao katika uingizaji wa watu kulingana na uwezo wa kumbi hizo, badala ya kuendekeza tamaa ya fedha kwa kujaza watu kupita kiasi. Vilevile, wazazi wawe makini na watoto wao na hasa disko toto, ili kuepuka ajali na matukio mengine yanayoweza kusababisha madhara juu yao.

Wananchi wanatakiwa kuwa makini
hususani watokapo kwenye makazi yao, wasiache nyumba wazi ama bila mtu
na pale inapobidi watoe taarifa kwa majirani zao. Wanapowatilia mashaka
watu wasiowafahamu wasikae kimya bali watoe taarifa haraka kwenye vituo
vya Polisi vilivyo karibu nao ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa
haraka.
Vilevile, Jeshi la Polisi
linawatahadhalisha wananchi kuwa makini na matapeli yanayotumia majina
ya viongozi, watu maarufu na wafanyabiashara wakubwa ili kujipatia pesa
na vitu mbalimbali. Matapeli hao wamekuwa wakitumia ujumbe mfupi wa simu
za mkononi kupata taarifa za mtu binafsi hatimae mtu huyo kuibiwa.
Ndugu wanahabari,
Kufuatia agizo la Mhe. Rais la kuwataka watu wote wanaomiliki silaha kinyume cha sheria kusalimisha silaha hizo, pamoja na watu wote wanaoingia ama kuishi na kufanya shughuli hapa nchini bila kufuata utaratibu (wahamiaji haramu) kutakiwa kuondoka au kuharalisha ukaazi wao, Jeshi la Polisi linawataka watu hao kuendelea kutekeleza agizo hilo la Serikali kabla ya Operesheni kabambe kuanza itakayoendeshwa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Vyombo Vingine vya Ulinzi na Usalama.

Aidha, baadhi ya watu hao tayari
wamekwishasalimisha silaha wanazozimiliki kinyume cha sheria na pia
baadhi ya wahamiaji haramu wameanza kuondoka hususani katika mikoa ya
Kagera na Kigoma. Hiyo ni hatua nzuri, tunawataka wale wote ambao bado
hawajatekeleza agizo hilo, waendelee kufanya hivyo haraka kabla ya muda
wa msamaha kumalizika.
Mwisho, napenda kuwahakikishia
wananchi kwamba, Jeshi la Polisi linatekeleza majukumu yake kwa
kuzingatia sheria za nchi na hivyo halitawajibika kumwonea huruma ama
upendeleo mtu yeyote atakayeenda kinyume na sheria.
NAWATAKIENI WATANZANIA WOTE SIKUKUU NJEMA YA
EID –EL-FITR
NAWATAKIENI WATANZANIA WOTE SIKUKUU NJEMA YA
EID –EL-FITR
Imetolewa na:-
Advera Senso- SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Advera Senso- SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Post a Comment