Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kabla ya kufungua mkutano wa
Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM mjini Dodoma Agosti 26,2013. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM wakiteta nje
ya ukumbi wa CCM wa White House mjini Dodoma Agosti 26,2013. Kutoka
kushoto ni Joyce Masunga, Raphael Chegeni na Samuel Sitta. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
ya ukumbi wa CCM wa White House mjini Dodoma Agosti 26,2013. Kutoka
kushoto ni Joyce Masunga, Raphael Chegeni na Samuel Sitta. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM wakiwa
kwenye Kikao chini ya Mwenyekiti Rais Jakaya Kikwete Agosti 26,2013.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
kwenye Kikao chini ya Mwenyekiti Rais Jakaya Kikwete Agosti 26,2013.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM wakiwa
kwenye Kikao chini ya Mwenyekiti Rais Jakaya Kikwete Agosti 26,2013.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
kwenye Kikao chini ya Mwenyekiti Rais Jakaya Kikwete Agosti 26,2013.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Katibu wa NEC Uchumi na Fedha
Zakhia Megji akibadilishana mawazo na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM
Taifa Mama Salma Kikwete katika ukumbi wa NEC, kabla ya kuanza kwa
kikao cha Halmashauri Kuu Dodoma leo, 26 Agosti 2013.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu
Abdulrahman Kinana akitoa taarifa za misiba iliyojiri, kabla ya kikao
akijaanza cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.
Wajumbe wa Halmashauri Kuu wakiwa
wamesimama kwa dakika moja kwa ajili ya kumuombea mjumbe mwenzao
aliyefariki ndugu Meja Jenerali Haji Makame Rashid.
Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa leo mjini Dodoma.
CCM YAZIDI KUWA IMARA ZAIDI
Kikao Cha Halmashauri Kuu ya CCM
Taifa kimemalizika jioni ya leo huku kukiwa na mabadiliko mbali mbali
makubwa kwenye chama hicho.
Kikao hicho ambacho kimeongozwa
na Mwenyekiti wake wa Taifa Jakaya Mrisho Kikwete kimemalizika kukiwa na
mabadiliko na mapendekezo mbali mbali, kikao hicho ambacho kimekaa kwa
siku tatu mfululizo kikitumia siku mbili nzika kujadili Rasimu ya Katiba
na maoni ya wana CCM .
Halmashauri hiyo pia imeridhia
uamuzi wa kufukuzwa uanachama Mansour Yussuf Himid kwa tuhuma za
Kushindwa kusimamia malengo na madhumuni ya chama na kutekeleza masharti
ya uanachama, kushindwa kutekeleza wajibu wa mwanachama na kukiuka
maadili ya Kiongozi wa CCM,Kuikana Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka
2010-2015 na kukisaliti chama.
Mansour alianza uanachama tarehe 7/4/1988 na ni mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki,wilaya ya Damani,Mkoa wa Magharibi Unguja.
katika hatua nyingine ya
Kimaadili sula la madiwani wa Bukoba bado halijafikiwa uamuzi ingawa
Kamati Kuu itakaa tena kesho tarehe 27 Agosti 2013 kufanya maamuzi ya
suala la Bukoba.
Kamati Kuu pia imependekeza
majina ya Makatibu wa Jumuiya,Ikiwemo Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT)
Amina Makilagi, Umoja wa Vijana CCM Ndugu Sixtus Mapunda, Wazazi Seif
Shaaban Mohamed .
Makatibu wapya wa Mikoa walioteuliwa ni Romuli Rojas John, Kaskazini Pemba Kassim Mabrouk Mbarak na Geita Mary Maziku.
Post a Comment