Baadhi
ya Wanamichezo wanaounda timu ya Polisi wakiwa katika mazoezi mepesi
wakati wa safari ya kuelekea katika jiji la Windhoek nchini Namibia.
Baadhi
ya Wanamichezo wanaounda timu ya Polisi wakiwa katika picha pamoja na
Askari wa Kikosi maalumu katika Jeshi la Polisi la Namibia
Baadhi ya Wanamichezo wanaounda timu ya Polisi wakiwa katika picha katika moja ya miji katika nchi ya Namibia.
Picha zote na Frank Geofray-Jeshi la Polisi-Windhoek Namibia.
Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi,Windhoek Namibia.
Hatimaye
timu ya Jeshi la Polisi Tanzania inayoshiriki Michezo ya Nane ya Umoja
wa wakuu wa majeshi ya Polisi kusini mwa Afrika (SARPCCO) nchini Namibia
imefika salama na imeanza mazoezi mepesi kwa ajili ya kujiandaa na
mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza jumatatu tarehe 19 mwezi Agosti
mwaka huu.
Timu
hiyo ambayo ni tishio katika michezo hiyo kutokana na historia yake ya
ushindi katika mashindano yaliyotangulia imekuwa kivutio kila inapopita
huku kila mmoja akitaka kusalimiana nayo.
Timu
hiyo inaundwa na wanamichezo 67 ambao wanacheza Mpira wa miguu
wanaume, Mpira wa pete Wanawake, Riadha wanaumwe na wanawake na mchezo
wa Vishale (Dats).
Michezo
hiyo itashirikisha Nchi kumi na nne (14) katika michezo mbalimbali na
lengo la michezo hiyo ni kujenga ushirikiano wa Majeshi ya Polisi kwa
nchi wanachama wa SARPCCO katika kukabiliana na uhalifu.
Post a Comment