Jengo la Bakwata lililopo kwenye makutano
ya Barabara ya Morogoro na Bibi Titi jijini Dar es Salaam, usiku wa
kuamkia juzi lilibolewa ghafla wakati mali za wapangaji zikiwemo ndani
na kusababisha hasara kubwa ya uharibifu na upotevu wa mali. Chanzo
kimoja cha habari eneo hilo kimedai kuwa Bakwata wamelibinafsisha jengo
hilo kwa mwekezaji kutoka nje ya nchi bila kuwashirikisha wapangaji
wake. Mwekezaji huyo ndiye anayedaiwa kutoa agizo la kubomoa jengo hilo
kabla ya notisi aliyoitoa kwa wapangaji hao kumalizika.
(PICHA : RICHARD BUKOS / GPL)
Post a Comment