Mkuu wa Chuo cha Uhasibu cha Arusha, John Nanyaro na Mkuu wa
Polisi wa Wilaya ya Arusha, Gillis Mroto, leo wanaanza kutoa ushahidi
katika kesi ya tuhuma za uchochezi inayomkabili Mbunge wa Arusha Mjini,
Godbless Lema.
Mashahidi wengine katika kesi hiyo ni, Mkaguzi wa Polisi Bernard Nyambanyana na mwenzake aliyetajwa kwa jina moja la Jane.
Hali kadhalika PC Godfrey na Joachim Mahanyu .
Wakili wa Serikali, Elinenya Njiro, alitaja mashahidi wengine watakaotoa
ushahidi wao mahakamani kuwa Faraji Mnepe, Benjamin Simkanga na Naibu
Hamidu, wote kutoka Chuo cha Uhasibu.
Lema anadaiwa kutoa maneno ya uchochezi kuwa Mkuu
wa Mkoa wa Arusha, Magessa Mulongo, alikwenda katika Chuo cha Uhasibu
cha Arusha, mithili ya mtu aliyekwenda kwenye send-off na kwamba hajui
chuo hicho kilipo wala mauaji ya mwanafunzi wa chuo hicho.
Wakili Njiro alidai kuwa mbunge huyo alitenda kosa
hilo Aprili 24 mwaka huu, akiwa katika eneo la Freedom Square ndani ya
Chuo cha Uhasibu na kwamba kitendo hicho kinapingana na kifungu cha 390
sura ya 35 ya sheria ya kanuni ya adhabu.
MWANANCHI
MWANANCHI
Post a Comment