![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiZ-F3C1qmaAw14R8fFf68pKSFqdvldtK1npMZRDT2im7qSQeGme8l0oYLJa8akymtgF3yppByvnRh1PlilBLncP6K1NXlVX2m5ULi5fEGJ_Hw_mDUQ6VtY1zzyYEfC9MD9qEIls7F61Sg/s640/1QWW.jpg)
Wakazi wa Mabibo External jijini Dar es Salaam wamekusanyika nje ya lango kuu la kuingia katika kanisa la Victorious Living lilipo katika eneo hilo kuushinikiza uongozi wa kanisa kuweka vifaa maaalum vya kuzuia kelele wakati wanapofanya ibada zao.
Wakazi wa Tabata External wamekusanyika nje ya lango kuu la kuingia katika
kanisa la Victory Living lilipo katika eneo hilo kushinikiza uongozi wa kanisa
kuweka vifaa maaalum vya kuzuia kelele wakati wanapofanya ibada zao kutokana na
kanisa hilo kutumia vyombo vyenye sauti kubwa ilihali kanisa hilo lipo katika
makazi ya watu.
Wakizungumza nje la kanisa hilo waumini hoa wamesema hawana shinda na
huduma zinazotolewa na kanisa hilo bali na namna ambavyo wanafungulia vyombo vya
muziki kwa sauti ya juu na hivyo wanajikuta usiku mzima hawalali hasa
wagonjwa.
Baadhi ya wakina mama wanaoishi jirani na kanisa hilo wamesema watoto wao
sasa wameanza kuonyesha hali ya utofauti kutokana na ukweli kuwa usiku hawalali
na mchana hawalali kutokana na makelele hayo na hivyo wanaziomba mamlaka huska
zione nini cha kufanya.
Akijibu tuhuma hizo mchungaji kiongozi wa kanisa hilo mchungaji John Saidi
amekiri kuwepo na malalamiko ya siku nyingine kati yake na wananchi wa eneo hilo
lakini amekuwa akijitahidi mara kwa mara kupata ufumbuzi wa kero hizo ikiwemo
kufuta baadhi ya huduma zinazotolewa kanisa lake, huku afisa mtendaji wa mtaa
huo bw henry mtogo akikiri kupokea malamamiko ya wananchi hao.CHSNZO ITV
Post a Comment