Na Rahimu Kambi, Handeni
BAADHI
ya wanafunzi wa kidato cha
nne shule ya Sekondary ya Kwamatuku, iliyopo Kata ya Kwamatuku, wilayani
Handeni, mkoani Tanga,
wameilalamikia shule yao kwa madai kuwa hawafundishwi kama
inavyostahili, hivyo kuhofia matokeo ya 'ziro' kuendelea kushika kasi
kila mwaka.
Mkuu wa Wilaya Handeni, Muhingo Rweyemamu
Wakizungumza kwa nyakati tofauti,
wanafunzi hao walisema ufundishaji kwenye shule yao sio mzuri, hivyo matokeo
kwenye ya ufaulu utaendelea kuwa ndoto.
“Hapa hakuna mwelekeo wowote, maana
tunafundishwa kwa kiasi kidogo mno na mara zote hatuambulii chochote cha maana
hali itakayotuweka sawa kwenye mitihahani yetu.
“Tunaomba serikali kwa kupitia Mkuu
wa wilaya Handeni, sambamba na wataalamu wa elimu hasa Afisa Elimu wa Sekondari
wilayani hapa kuliangalia suala hili kwa kina,” alisema.
Wanafunzi hao walitolea mfano
mwalimu wa anayefundisha somo la Kingereza kutowajibika ipasavyo kwa ajili ya
kuwaandaa wanafunzi hao jambo linalowafanya wafeli katika mtihani wa Taifa kila
mwaka.
Akizungumzia tuhuma hizo, Kaimu
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo ya Kata ya Kwamatuku, Godfrey Bendera, alisema madai
hayo hayana ukweli na yametolewa kwa sababu wanazojua wenyewe.
“Shule yetu ina bodi na ina uongozi
mzuri, hivyo inashangaza kwanini masuala hayo yasiibuke kwanza kwetu na kuanzia
katika ngazi za habari na kuibua maswali.
“Kwanza mimi sio msemaji wa shule
hii, lakini katika suala hilo nabaki nashangaa na kujiuliza maswali lukuki,
ukizingatia kuwa katika shule yetu utaratibu ni mzuri mno,” alisema Bendera.
Shule ya Kwamatuku, inatumiwa na
vijiji vya Komsala, Kweingoma, Nkhale, Kwamatuku na wengineo, ikiwa ni kati ya
zile zilizojengwa kwa wingi katika Taifa hili ili zitowe fursa ya kuwapatia
elimu ya sekondari Watanzania.
Post a Comment