Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WANANCHI WAMHUSISHA RAIS KIKWETE MGOGORO WA ARDHI BAGAMOYO

 



Katibu wa wamiliki wa mashamba na makazi wa kijiji cha Buma, Gumbo Majibwa akisoma taarifa kwa wananakijiji wenzake, huku pembeni yake Mwenyekiti Hassani Tenela akimsikiliza kwa makini katika mkutano wao wa kupinga kutaka kuchukuliwa kwa maeneo yao ili kumpish mradi wa hospitali ya kimataifa inayodaiwa itamilikiwa JWTZ
Mmoja wa wamiliki wa mashamba na makazi wa kijiji cha Buma akiandikisha jina katika karatasi ya mahudhurio

Sehemu ya wahudhuriaji wakisikiliza kwa makini taarifa juu ya sakata la kutaka kuporwa kwa maeneo yao


Wamikili wa mashamba na makazi kijiji cha Buma, wilaya ya Bagamoyo wakiwa kwenye mkutano wao uliofanyika juzi Jumamiosi
Mpaka kieleweke hapa....Ardhi yetu anaitaka Rais au Jeshi? wanaulizana wamamiliki wa ardhi ya kijiji cha Buma

Najiorodhesha ili wasiseme sikuwepo!
Khadija Omary mmoja wa wanaomiliki ardhi katika kijiji cha Buma akitoa hoja na kuuliza maswali katika mkutano wao wa Jumamosi.

Viongozi wa Kamati waliosimama kando ya gari wakisoma taarifa kwa wamiliki wenzao kuhusu sakata la kutaka kuporwa kwa ardhi yao,.

Na sisi tumo mpaka kieleweke!

Hata iwe vipi ardhi yetu haiwezi kuchukuliwa kienyeji

Husna Mohammed naye hakuwa nyuma kutoa maoni yake. Mwanamama huyo ni mmoja wa watu sita walioteuliwa katika kamati maalum ya kwenda kumuona Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Dk Shukuru Kawambwa ili kujua ardhi yao inachukuliwa na mwekezaji aliyetafutwa na Rais au ni JWTZ

"Tujiadharini isije kuna matapeli wanalitumia jeshi na jina la Rais kutaka kupora eneo leo. Hospitali gani inayojengwa katika eneo la ekari 1500? Dk Ally Ponza alihoji katika makutano huo
Tupo nanyi mwanzo mwisho mpaka kieleweke, hatukubali kirahisi kuachia ardhi yetu.

Frank Lyimo naye alitaka upatikane uthibitisho juu ya nani anayetaka kuchukua ardhi yao ili wasije wakambebesha lawama Rais Kikwete bure wakati kumbe hajui chochote kinachoendelea katika kijiji cha Buma.

Tupo pamoja

Katibu Gumbo Majubwa akitoa ufafanuzi baada ya kuulizwa na wanakijiji wenzake

Umoja ni nguvu! Hapa mwanzio mwisho mpaka tujue ukweli

Mwenyekiti wa kamati Hassan Tenela akifafanua jambo kwa wamiliki wenzake kuhusu ufuatuiliaji wao juu ya sakata la kutaka kuporwa ardhi yao.

"Jamani, tumeelezwa jeshi limetumwa tu kusaka ardhi, lakini mwekezaji ametafutwa na Rais alipokuwa nje ya nchi, lakini cha ajabu Mbunge wetu hajui na wala bajeti ya kulipwa fidia kwa kuporwa ardhi haipo kwenye Bajeti ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ya 2013-2014' Mwenyekiti Hassan Tenela akiwafafanulia wenzake mahali alipofikia
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top