WANANCHI
wa Kata ya Kikombo, Juni 6, walimtimua Mtendaji wa Kijiji na Kaimu
Mtendaji wa Kata, Wello Dede, kwenye mkutano wa hadhara, wakimtuhumu kwa
ubadhirifu wa fedha akibebwa na viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM).
Hata
hivyo, Dede alivituhumu vyama vya Chadema na CUF kuwa vomechochea
atimuliwe, wananchi wakikanusha kuwa wamemtimua kutokana na kuchoshwa
naye kwa kulamba Michango wanayochangishwa bila kusomewa mapato na
matumizi kwa miaka miwili sasa.
Wakizungumzia
hatua hiyo, wananchi pia wamedai hawawezi kushiriki kazi zozote za
Maendeleo wala kutoa michango yoyote ya kazi hizo hadi wasomewe mapato
na Matumizi ya Kijiji na Kata ya muda uliopita, la sivyo kijijini hapo
hapatatosha kwake!.
Akikiri
kutimuliwa Mtendaji huyo alidai, anachojua Wanachama wa CHADEMA na wale
wa CUF, ndio waliomtimua na si wa CCM, akisema wanarejea kauli yao ya
awali kuwa hawamtaki, na aking’ang’ania atapata Mkong’oto anaoutaka.
”Mwandishi;
Kazi zetu hizi si za kupendwa, ninachofahamu muda wangu wa
kubadilishiwa Kituo cha Kazi umefika, na kama nitang’ang’ania kukaa hapa
ni kweli ninaweza kuumizwa vibaya”.alisema Dede akijigamba ni kutokana
na kuhimiza kwake Maendeleo bila woga.
“Wananchi
hawa nawashangaa sana, nikifuatilia Michango na Kazi za Maendeleo wao
wanadai ni CHADEMA au CUF wamesusia maendeleo! Kwani tukiandikisha
Wanafunzi shuleni, tunawauliza kama ni huyu CCM, CUF au
Chadema?”.alisema Dede akidai ndiyo maana Nyerere alikataa vyama vingi.
Utetezi
wa Dede ulipingwa vikali na wananchi wakidai, amefuja michango ya
ujenzi wa Shule ya Msingi Kikombo, Michango ya Wafugaji kwa ajili ya
Josho, huku wakidai kitimutimu kingine, kinamsubiri Mwenyekiti wake,
Petro Kusena (CCM).
Katika
Mkutano wa hadhara wa CHADEMA hivi karibuni, kiliwananga Viongozi hao
kwa wananchi kwa kutoezeka Shule ya Msingi iliyoezuliwa Miaka miwili
iliyopita. Licha ya Polisi Kata siku hiyo kumkwida na kumnyang’anya
Kipaza sauti Katibu wa Chadema (W), Jella Mambo; Dede na Kusena
walikanusha Kulamba fedha hizo.
Post a Comment