Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na
Jenerali David Musuguli Mkuu wa Majeshi Mstaafu wakati alipomtembelea na
kumjulia hali Mjini Butiama leo, wakati akiondoka wilayani humo
kuelekea Mugumu Wilaya ya Serengeti kuendelea na ziara yake ya
kuimarisha chama na kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama
hicho, Jenerali Musuguli alionekana kuwa na bashasha wakati alipomuona
Abdulrahman Kinana pengine ni kutokana na utendaji kazi wa katibu mkuu
huyo wa CCM, ambapo alisikika akisema huyu ni kijana wangu huku wakiwa
wameshikana mikono wakiingia ndani kwa mazungumzo ya faragha.PICHA NA
KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-MUGUMU SERENGETI
Jenerali
David Musuguli Mkuu wa Majeshi Mstaafu akisalimiana na Nimrod Mkono
Mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini kushoto ni Nape Nnauye Katibu wa
Itikadi Siasa na Uenezi CCM.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo
wakati alipokuwa akizungumza na Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali David
Musuguli nyumbani kwake Butiama.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo
katika mazungumzo hayo huku Mkuu wa Wilaya ya Butiama Angelina Mabula
akisikiliza kwa makini.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana na Jenerali David
Musuguli wakiingia ndani huku wakiwa wameshikana mikono.
Jenerali David Musuguli akipiga picha ya kumbukumbu na Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana, na maofisa kadhaa
ambao ameongozana nao katika msafara huo, kushoto ni Mbunge wa jimbo la
Musoma Vijijini Nimrod Mkono.
Jenerali David Musuguli akipiga picha ya kumbukumbu na waandishi wa habari, kushoto ni Nimrod Mkono Mbunge wa Musoma vijijini.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akiagana na Jenerali David Musuguli wakati alipomtembelea nyumbani kwake leo.
Jenerali David Musuguli akiagana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi Siasa na Uenezi huku wakionekana kufurahia jambo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasili katika kata ya Isenye wilaya ya Serengeti Akisalimiana na na wana CCM walipokuwa wakimlaki leo
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia kikundi cha ngoma wakati kikitumbuiza.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akivishwa skafu na
wanafunzi wa shule ya sekondari ya Nata wilayani Serengeti leo.
Wimbo wa taifa
Wanafunzi wa Shule ya sekondari Nata wakiimba wimbo wa taifa.
Mwalimu
Mwema Machage wa Darasa la Kompyuta katika shule ya sekondari ya Nata
akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na ujumbe
wake wakati alipokagua shule hiyo
Mwalimu
Peter Simon wa shule ya Sekondari ya Nata wilayani Serengeti akielezea
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana jinsi wanavyowafundisha
wanafunzi wake somo la sayansi wakati alipotembelea maabara ya shule
hiyo.katikati ni mwanafunzi wa kidato cha nne Silvesta Joseph
mwanafunzi wa kidato cha nne Silvesta Joseph akitoa maelezo mbele ya
Katibu Mkuu wa CCM kuhusu wanafunzi hao wanavyojifunza jinsi ya
kutengeneza sabuni katika maabara hiyo ya shule.
Wananchi wakimpungia mkono Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
Kinana akizungumza na wananchi katika kata ya Isenye
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mgorole na
Mzee Nyangarisi Kumari kuwa mmoja wa wazee wa heshima wa kimila wa
kabila la Kiikoma tukio hilo limefanyika katika kata ya Bukore.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana baada ya
kutawazwa mzee wa heshima wa kabila la Kiikoma katika kijiji cha Bukore
wilayani Serengeti
Post a Comment