Akitoa hukumu hiyo katika kikao chake kinachoendelea Nzega iliyochukua zaidi ya dakika 45, Jaji Amiri Mruma alisema mahakama imeridhika na ushahidi uliowasilishwa dhidi ya mtuhumiwa James Okoko (51) mkazi wa Nzega mjini.
Jaji huyo alisema kutokana na kukithiri kwa vitendo vya mauaji ya kikatili pamoja na kushambulia kwa mapanga bila sababu na kujichukulia sheria mkononi ametoa hukumu hiyo ili iwe fundisho kwa watu wenye nia kama hizo.
Awali wanasheria wa serikali Ildephonce Mkandara, Grace Muwange na Monica Mlao waliiambia mahakama hiyo kuwa mtuhumiwa alimpiga mama yake mzazi Catherine Mihambo hadi kufa kwa kutumia fimbo na stuli aliyompiga nayo kichwani baada ya kukatazwa kula chakula cha mchana kutokana na utovu wa nidhamu, tukio hilo lilitokea Septemba 23 mwaka 2008.
Post a Comment