Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

GARI LA OPERESHENI KIMBUNGA LAPINDUKA NA KUUA ASKARI WATATU

 


MIILI YA ASKARI  IKIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA KAHAMA
Askari Polisi watatu wa operesheni Kimbunga ya kusafisha wahamiaji haramu nchini, wamefariki dunia jioni hii mjini Kahama kufutia ajali ya gari walilokuwa wakisafiria kutoka Muleba mkoani Kagera kuelekea makambako mkoani Njombe.
Marehemu hao waliotambulika kwa majina ya Kopolo Fred,PC Subian na PC Michael wote ni askari wa kituo cha Polisi Makambako, na mauti yamewafika baada ya gari nambari PT 0776 Land Rover Diffender kuacha njia na kupinduka.

Ajali hiyo imetokea katika eneo la Sungamile Kata ya Kagongwa wilayani Kahama wakati dereva wa gari hilo PF3270 PC Yusuph, akijaribu kumkwepa Bibi Kizee mmoja huku gari likiwa kwenye mwendo kasi hali iliyosababisha kumshinda na kupinduka.


Blog imeshuhudia Majeruhi wanane wakilazwa katika Hospitali ya wilaya ya Kahama wakiwemo askari polisi sita na Afisa uhamiaji wawili, huku magari yanayosafirisha askari kurudi vituoni kwao yakizuiliwa kuendelea na safari na kulala Kahama.


Kumbukumbu za kipolisi pia zimeonesha kuwa hapo jana jioni askari wengine walipata ajali katika kijiji cha Igusule wilayani nzega ambapo askari 4 wamelazwa katika hospitali ya wilaya Kahama huku mmoja akiwa na hali mbaya.


Oparesheni Kimbuga ni utekelezaji wa agizo la Rais Jakaya Kikwete, la kuwaondoa wahamiaji haramu nchini, ambapo vikosi vya ulinzi kwa pamoja viliunda kikosi kimoja na kufanya kazi nchini kote.
 
kijukuu blog
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top