Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amesema kwa sehemu kubwa utekelezaji wa maendeleo ya millenia umefanikiwa nchini mwake licha ya kwamba yako malengo ambayo bado hayajafanikiwa mathalani usafi wa mazingira na kuanisha mipango iliyopo katika kuyatimiza.
Katika mahojiano maaluma na Joseph Msami wa Idhaa ya Kiswahili ya radio ya Umoja wa Mataifa , Rais Kikwete amesema nchi zilizoendelea zimekuwa zikisita kutimiza lengo namba nane linalowataka watoe asilimia saba ya pato la taifa ambapo akitoa mfano kwa nchi kama Marekani amesema ni kiasi kikubwa na hivyo kutotomizwa jambo hilo kwa ujumla linachelewesha utekelezaji wa malengo hayo.
Bofya kitufe cha pleya umsikilize hapo chini
on Monday, September 30, 2013
Post a Comment