Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, mkoani Manyara, Anatory Choya akiwa amewapigia wananchi magoti kwa maana ya kuonyesha unyenyekevu
Mbulu. Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, mkoani Manyara,
Anatory Choya, amesema kuwa aliwapigia magoti wananchi wa Kijiji cha
Hydom, ili kuonyesha unyenyekevu kwa wananchi hao aliodai walionekana
kujazwa maneno ya uchochezi na wanasiasa ili wavuruge amani .
Alisema kutokana fujo zilizofanywa na baadhi ya
wananchi hao katika mkutano wa hadhara uliofanyika majuzi, kwa nafasi
yake angeweza kuagiza hata Jeshi la Polisi kuwadhibiti watu, lakini
misingi ya dini yake haimruhusu kumdhuru mtu zaidi ya kumwonyesha
unyenyekevu.
Alisema hali hiyo ndiyo iliyomfanya kuamua kupiga magoti na kumshtakia Mungu.
“Mimi ni mkristo, unyenyekevu ndiyo nguzo pekee ya
kuonyesha upendo na kudumisha amani. Ningeweza kuagiza polisi
wawadhibiti, lakini sioni sababu kwa kuwa hiyo siyo misingi ya utawala.
Ndiyo maana nikaona bora nitumie njia nyingine ya kumshirikisha Mungu
mbele yao,”alisema Choya na kuongeza:
“Wanasiasa wamekuwa wakipandikiza chuki kwa
wananchi kwa makusudi kwa lengo la kuvuruga amani lakini kwa kumweka
Mungu mbele nina imani tutafanikiwa ili siku moja tusije tukaingia
kwenye mkumbo wa Syria na Misri”
Choya alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akizungumza
na Mwananchi Jumapili, siku chache baada ya kitendo chake cha kupiga
magoti mbeye ya wananchi kwenye mkutano wake wa hadhara uliofanyika
katika Kijiji cha Haydom.
Mkuu huyo wa wilaya alidaiwa pia kuwalaani baadhi
ya wakazi wa Kijiji cha Haydom kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kumdharau
na kutofuata maagizo yake, wakati yeye amewasaidia katika kutatua
migogoro mbalimbali waliyokuwa nayo.
Tukio hilo la kusikitisha lilijitokeza baada ya
wananchi wa kijiji hicho kupinga agizo la Choya, lililowataka kufanya
uchaguzi wa kaimu mwenyekiti wa kijiji hicho, kabla ya kufanya uchaguzi
mdogo, ambapo walipinga kwa kudai kuwa hakuna sheria hiyo.
Mmoja wa wananchi hao alilumbana na mkuu huyo wa
wilaya mbapo Choya alijibu; “Nami nitarudi kwetu." Naye Tikin akasema
tena: “Unasema utarudi kwenu Biharamulo wakati hawakutaki kwani
ulifukuzwa ubunge?”
Maneno hayo yalionyesha kumkwaza Choya ambapo
alipiga magoti huku machozi yakimlenga na kumwomba Mungu afanye jambo
kwa watu wa Haydom kwani wanamdharau kabla ya kujitokeza wazee watatu wa
Haydom na kumwomba msamaha mkuu huyo wa wilaya
Post a Comment