Kocha Mkuu wa timu ya taifa (Taifa Stars) Kim Poulsen.
Mahmoud Ahmad Arusha
Kocha
Mkuu wa timu ya taifa (Taifa Stars) Kim Poulsen anatarajiwa kuwa mgeni
rasmi kwenye ufunguzi wa Ligi ya vijana chini ya umri wa miaka 15 ya
Moivaro Youth League. Ligi hiyo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi siku ya
Jumamosi ya tarehe 28 mwezi huu katika viwanja vya International
school.
Akizungumza
na vyombo vya habari jijini Arusha, Mratibu wa ligi hiyo, Alfred Itael
alisema kuwa ligi hiyo itakuwa ya nyumbani na ugenini na kuwa
itazishirikisha timu zaidi ya 30 za vijana chini ya umri wa miaka 15
inadumu ndani ya miezi mitatu.
Bw.
Itael ametoa wito kwa wazazi na vijana kushirikiana katika kuendeleza
soka la vijana kwani Michezo ni sehemu ya kujenga mwili na pia ni ajira
kwa vijana lakini amewataka vijana kutobweteka na michezo na kuacha
kusoma kwani mpira wa sasa unaendana na elimu.
Post a Comment