Mhandisi
Mkazi Eng. Peter Gibson (aliyenyoosha mkono) kutoka Kampuni ya Nicholas
O’ Dwyer & Partner akimpatia maelezo Waziri wa Ujenzi Mhe. John
Pombe Magufuli, kuhusu utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa barabara ya
Mbeya – Chunya. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Abbas Kandoro.
Waziri
Wa Ujenzi Mhe. John Pombe Magufuli (katikati aliyeinama) akiangalia
mamendeleo ya ujenzi wa barabara ya Mbeya – Chunya. Kushoto kwa Waziri
Magufuli ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Abbas Kandoro.
Waziri
Wa Ujenzi Mhe. John Pombe Magufuli (aliyetangulia) akikagua mamendeleo
ya ujenzi wa barabara ya Mbeya – Chunya. Nyuma ya Waziri Magufuli ni
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Abbas Kandolo.
Mhandisi
Mkazi Eng. Peter Gibson (kushoto) kutoka Kampuni ya Nicholas O’ Dwyer
& Partner akimpatia maelezo Waziri wa Ujenzi Mhe. John Pombe
Magufuli, kuhusu uwekaji wa lami katika barabara ya Mbeya – Chunya
sehemu kati ya Lwanjilo na Chunya.
Mkandarasi
aliyekuwa amepewa kazi ya kujenga barabara ya kuanzia Mbeya mjini hadi
Lwanjilo kwa kiwango cha lami anatakiwa kuilipa Serikali ya Tanzania
Shilingi bilioni 16 baada ya kushindwa kesi. Kampuni ya Kundan Singh ya
kutoka Kenya iliachakazi za ujenzi kinyume na mkataba na kukimbilia
mahakamani ambako imeshindwa na kutakiwa kulipa kiasi hicho cha fedha.
Wananchi
wa Chunya walijulishwa uamuzi huo na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt.
John Pombe Magufuli alipokuwa akiongea katika mkutano wa hadhara mjini
Chunya. “Baada ya mradi huu kusimama kwa muda mrefu kusubiri maamuzi ya
mahakama hatimaye mradi huu sasa unaendelea na mkandarasi aliyetupeleka
mahakamani ameadhibiwa kutulipa shilingi bilioni 16” alibainisha
Mheshimiwa Magufuli.
Wizara
ya Ujenzi inaendelea kutekeleza ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami
kati ya mji wa Mbeya na Chunya kupitia Lwanjilo. Mradi huu umegawanywa
katika sehemu mbili ukianzia Mbeya mjini hadi Lwanjilo yenye urefu wa
kilometa 36 na sehemu ya pili inaanzia Lwanjilo hadi Chunya pia ikiwa na
urefu wa kilometa 36.
Mheshimiwa
Magufuli aliendelea kufafanua kuwa tayari kuanzia mwezi Desemba 2010,
mkandarasi mpya alikwishapatikana na atakamilisha kazi ambazo ziliachwa
na mkandarasi wa awali ambaye aliingia mkataba mwaka 2007 na kisimamisha
kazi mwaka 2009. Kampuni ya China Communication Construction Company
(CCCC) imeshinda zabuni ya kumalizia ujenzi wa sehemu hii ya kwanza
kutoka Mbeya mjini hadi Lwanjilo kwa gharama ya Shilingi bilioni 55.4.
Mkandarasi huyu baada ya kuwa ameongezewa muda kutokana na mabadiliko ya
viwango vya kazi sasa anatakiwa awe amekamilisha mradi huu kabla ya
mwezi Desemba 2014.
Akizungumzia
sehemu ya pili ya mradi huo ambayo inaanzia eneo la Lwanjilo hadi
Chunya, inayojengwa na Kampuni hiyo hiyo ya China Communication
Construction Company (CCCC), Mheshimiwa Magufuli alimtaka mkandarasi
kuwa amekamilisha kazi zote ifikapo mwezi Aprili mwaka 2014 kama mkataba
unavyomuelekeza. Sehemu hii inajengwa kwa gharama ya Shilingi bilioni
40.2.
Kuchelewa
kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa barabara kati ya Mbeya na Chunya
kumekuwa kukilalamikiwa kwa kipindi kirefu. Hivyo kupatikana kwa
mkandarasi wa kumalizia kazi kwa sehemu ya kwanza kumeleta faraja kubwa
kwa wananchi wa maeneo hayo ambao wengi wao waliitikia vyema wito wa
kubomoa majengo yao yaliyo ndani ya hifadhi ya barabara ili kupisha
ujenzi mradi huo.
Post a Comment