Marehemu Privite Hugo Barnabas Mugo, enzi za uhai wake.
Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue akisaini kitabu…
Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davis Mwamunyange (wa pili kutoka kushoto)
akiwasili katika Viwanja vya Lugalo leo saa asubuhi kwa ajili ya kuaga
mwili wa askari wake.
Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Ombeni Sefue ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi akiwasili katika viwanja hivyo.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akisalimiana na baadhi ya viongozi alipowasili katika Viwanja vya Lugalo.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akiwa na Balozi wa Tanzania
nchini China na Luteni Jenerali Mstaafu Shimbo, nyuma yao ni Balozi wa
Tanzania nchini DRC.
Mwili wa marehemu ukipelekwa kwenye gari tayari kwa safari kuelekea mkoa wa Kilimanjoro kwa ajili ya mazishi.
MAJONZI, vilio na simanzi vilitawala leo
katika Viwanja vya Jeshi, Lugalo jijini Dar es Salaam pale mwili wa
Private Hugo Barnabas Mugo ulipowasili kwa ajili ya kuagwa.
Hugo alifariki dunia Septemba 18 mwaka huu baada ya kulipukiwa na bomu nchini DRC alipokuwa katika kikosi cha kulinda amani. Baada ya kulipukiwa na bomu alipelekwa Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu.
Hafla ya kumuaga iliongozwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Sifuni Ombeni na JWTZ liliongozwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyage.
Katika hotuba yake kwenye hafla hiyo, Jenerali Mwamunyange amesema kuwa kwa mara nyingine Tanzania imepata pigo kubwa kwa kumpoteza askari wake huyo shupavu.

(PICHA/HABARI: NA HARUNI SANCHAWA / GPL)
1 comments:
RIP our classmate
ReplyPost a Comment