Waziri
wa Katiba na Sheria (Kulia), Mathias Chikawe akijandaa kuvaa kofia ya
kujikinga (Helmet) kabla ya kuanza ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa
jengo la Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) linaloendelea
kujengwa katika mtaa wa Makunganya jijini. Kushoto ni Afisa Mteandaji
Mkuu wa RITA, Phillip Saliboko.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) Phillip
Saliboko akitoa maelezo mafupi kwaWaziri wa Katiba na Sheria, Mathias
Chikawe (kulia) kabla ya kukagua jengo lao lililopo mtaa wa Makunganya
jijini.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya ushauri wa Ujenzi ya Undi
Consulting Group Limited, Phillip Makota akitoa maelezo kwa Waziri wa
Katiba na Sheria, Mathias Chikawe katika moja ya ‘floor katika jengo
linaloendelea kujengwa la RITA.
Waziri
wa Katiba na Sheria , Mathias Chikawe akifafanua jambo mara baada ya
kumaliza kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la RITA. Kulia ni Afisa
Mtendaji Mkuu wa RITA, Phillip Saliboko
Na Mwandishi Wetu
Waziri
wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe amesema kuwa amefuraishwa na
manedeleo ya ujenzi wa jengo la Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini
(RITA) na kutangaza rasmi kuwa atamuomba Rais Drk Jakaya Mrisho Kikwete
kulifungua rasmi jingo hilo mwishoni mwa mwaka huu.
Waziri
Chikawe alisema hayo wakati alipotembelea maendeleo ya ujenzi wa jingo
hilo lenye ghorofa 27 katika mtaa Makunganya jijini karibu na ukumbi
maarufu wa burudani wa Club Billicanas.
Alisema
kuwa amefuraishwa na kitendo cha kampuni za kizalendo kuhusika kwa
kiasi kikubwa katika kufanikisha wa jingo hilo ambalo litakuwa la pili
kwa urefu ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.
Alifafanua
kuwa ukiondoa mkandarasi mkuu, kampuni ya China Railway Jianchang
Engineer (T) Limited, kampuni nyingine zilizobaki katika kufanikisha
ujenzi huo ni za kitanzania.
Kampuni
hizo ni Undi Consulting Group Limited ambayo inahusika na mradi wa
ujenzi huo, Design Concern (iliyofanya kazi ya kubuni na kuchora ramani
ya jengo) na kampuni ya Kamu Cost Engineering Centre ambayo ilifanya
savei ya ujenzi wa jengo.
Kampuni
nyingine ni Unicool (East Africa) Company Limited, Sec (East Africa)
Company Limited, Techno Image Limited na Derm Electrics (T) Limited.
“Haya
ni maendeleo makubwa kwa Tanzania kuona makampuni ya kizalendo
yanatumika katika kufanikisha ujenzi wa majengo ya kisasa kama hili la
RITA, ni jengo lenye ubora wakimtaifa, nimevutiwa na maendeleo ya mradi
na nitamuomba Mheshimiwa Rais, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kuja kulifungua
rasmi,” alisema Chikawe.
AfisaMtendajiMkuuwa
RITA, Phillip Saliboko alisema kuwa ujenzi wa jengo hilo umegharimiwa
na Mfukowa Hifadhi ya Jamii wa (NSSF) na utagharimu shs 35.86 Bilioni
ambazo zitalipwa kwa kipindi cha miaka nane kwa mujibu wa makubaliano
yao.
Saliboko
alisema kuwa mbali ya ofisi yao ambayo kwa sasa ipo Upanga kuhamia
hapo, jengo hilo pia litapangishwa kwa makampuni na taasisi nyingine
kama kitega uchumi chao.
“Jengo
letu ni la kisasa, lina vifaa maalum vya kuzuia ajali za moto ikiwa
pamoja na milango ambayo moto hauwezi kupenya na kusambaa, kwa kweli
tumewekeza kwa kiasi kikubwa na kwa kuzingatia usalama wetu na wapangaji
wengine,” alisema Saliboko.
Post a Comment