“PRESS RELEASE” TAREHE 21. 09. 2013.
WILAYA YA RUNGWE – AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU
NA KUSABABISHA KIFO.
NA KUSABABISHA KIFO.
MNAMO
TAREHE 20.09.2013 MAJIRA YA SAA 12:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA NDAGA
WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA. GARI T.565 AINA YA TOYOTA COASTER
LIKIENDESHWA NA DEREVA SHABAN S/O IDDI, MIAKA 32, MKINGA, MKAZI WA
TUKUYU LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU MTOTO KALEBO S/O EZEKIA, MIAKA 5,
KYUSA, MKAZI WA KIJIJI CHA NDAGA NA KUSABABISHA KIFO PAPO HAPO.
CHANZO MWENDO KASI. MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA
KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI. DEREVA AMEKAMATWA, TARATIBU ZA KUMFIKISHA
MAHAKAMANI ZINAFANYWA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA
MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA MADEREVA
KUWA MAKINI WANAPOENDESHA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA
USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
|
MNAMO
TAREHE 20.09.2013 MAJIRA YA SAA 15:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA
MBANGALA WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA
WALIMKAMATA PAUL S/O MAHAGA MIAKA 22, MSUKUMA, MKULIMA, MKAZI WA
MBANGALA AKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA TATU
[03]. MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA MTUMIAJI WA POMBE HIYO. TARATIBU
ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII
KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] KWANI NI KINYUME CHA
SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
Signed by:
[DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Post a Comment