Mratibu wa Tamasha la Handeni Kwetu 2013, Kambi Mbwana, ambaye pia ni Mmiliki wa mtandao huu wa Handeni Kwetu Blog, pichani.
Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya
Handeni, Dr Khalfany Haule, akizungumza na Handeni Kwetu, ofisini kwake
muda mchache baada ya kuruhusu Tamasha la Handeni Kwetu kufanyika
wilayani humo, Desemba 14 mwaka huu.
Mkuu wa Wilaya Handeni, Muhingo
Rweyemamu, akizungumza na Handeni Kwetu Blog, jana ofisini kwake
wilayani Handeni, mkoani Tanga.
TAMASHA
la Utamaduni lililopewa jina la ‘Handeni Kwetu 2013’ linatarajiwa
kufanyika Desemba 14 mwaka huu wilayani Handeni, mkoani Tanga, likiwa na
lengo la kutangaza sekta ya utalii na utamaduni wilayani humo.
Handeni
Kwetu linafanyika kwa mara ya kwanza tangu kuasisiwa kwa wilaya hiyo
inayoongozwa kwa sasa na Mkuu wa wilaya Muhingo Rweyemamu.
Akizungumza
jana wilayani Handeni, Mratibu wa Tamasha hilo, Kambi Mbwana, alisema
wameamua kuandaa tamasha hilo ili kushirikiana na wadau wote kutangza
utamaduni nchini Tanzania.
Alisema
kadri siku zinavyozidi kusonga mbele, jamii nyingi zimekuwa zikiiga
tamaduni za watu hasa kutoka nje ya nchi, jambo linaloleta mkanganyiko
wa kiasi kikubwa.
“Tumeamua
kuandaa tamasha hili kwa kupitia kampuni ya Raha Company and
Entertainment, ambapo lengo kubwa ni kuhakikisha kuwa linafanyika kwa
mafanikio makubwa.
“Mipango
kabambe inawekwa kulifanya tamasha letu liwe na mguso wa aina yake,
ukizingatia kuwa linafanyika mwishoni mwa mwaka, hivyo tunaamini watu
wengi watashiriki na sisi, hasa wale waliokuwa kwenye kipindi cha
mapumziko ya mwisho wa mwaka,” alisema Mbwana.
Mbali
na kufanya tamasha la Utamaduni wilayani humo, pia kutafanyika mchezo wa
riadha kwa ajili ya kuzindua hamasa katika mchezo huo wilayani Handeni,
mkoani Tanga.
Post a Comment