Sura ya tovuti ya SHUWASA inavyoonekana baada ya kufunguliwa
Mhe.Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Ally N.Rufunga akizindua tovuti ya
Mamlaka ya Maji safi na Maji Taka Mkoani
Shinyanga(SHUWASA)
Mkuu wa Mkoa Mhe.Rufunga akitoa nasaha
kwa wajumbe wa bodi mpya ya Maji ya Mkoa wa Shinyanga baada ya
kuwakabidhi vitendea kazi.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Maji taka Mkoa wa Shinyanga Ndg.
Sylivester Mahole akitoa taarifa fupi ya Mamlaka hiyo kabla ya Mgeni
rasmi Mkuu wa Mkoa kuzindua Bodi mpya ya maji na kuvunjwa Bodi ya
zamani.
Mkuu
wa Mkoa akizindua Mkataba wa Huduma kwa Mteja wa Mamlaka ya Maji safi
na Maji taka mkoani Shinyanga,kushoto ni Mkuu wa wilaya ya
Shinyanga Mhe.Anna Rose
Nyamubi.
Akimpongeza Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Maji ya Mkoa wa Shinyanga Brigedia Jenerali Mstaafu Dkt. Yohana Balele
---
Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.Ally N. Rufunga amezindua Bodi mpya ya Maji ya
Mkoa wa Shinyanga katika halfa fupi iliyofanyika Alhamisi hii, kwenye
ofisi za Mamlaka ya Maji safi na maji Taka mkoani Shinyanga (SHUWASA).
Katika
hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa amewataka wajumbe wa Bodi mpya
inayoongozwa na Mwenyekiti wake Brigedia Jenerali (Mstaafu),Dkt.Yohana
Balele,kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoikabili idara ya maji
ambazo alizitaja kuwa ni miundombinu hafifu hasa mabomba,
uchache wa wateja wanaotumia maji na wateja sugu wa kulipa madeni ya
maji.
Wajumbe wengine wa bodi mpya ni
Dkt.Anselm Tarimo (Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga),Bw. Festo Kang'ombe (
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga),Dkt.Ramadhan Kabala(Mganga Mkuu wa
Mkoa) na Bw.Fred Shoo(Mfanyabiashara). Wengine ni Paulina
M.Limbe,Mhe.Mourice Mugini,Dkt. Justus Rwetabula na Sylivester Mahole
ambaye ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Maji taka (SHUWASA)
Aidha, Mhe.Mkuu wa Mkoa amevunja bodi ya zamani ambayo imemaliza muda wake baada ya kufanya kazi kwa miaka mitatu.
Katika
hafla hiyo pia,Mkuu wa Mkoa amezindua baraza la Wafanyakazi wa mamlaka
ya Maji,amefungua tovuti ya Mamlaka ya maji safi na Maji taka (SHUWASA)
pamoja na kuzindua mkataba wa huduma kwa mteja.
Post a Comment