Naibu
Makamu Mkuu wa Chuo,Taalum kutoka chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof.
Makenya Maboko(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari(hawapo
pichani) kuhusu mafanikio ya utekelezaji ya Mradi wa Sayansi,Teknolojia
na Elimu ya Juu(STHEP) wakati wa mkutano uliofanyika leo jijini Dar es
Salaam.Kulia ni Kaimu, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho,Utawala Prof.
Boniventure Rutinwa.
Makamu
Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania,Rasilimali Prof. Marten
Victor(kushoto) akiwaeleza waandishi wa habari(hawapo pichani) jinsi
mradi wa Sayansi,Teknolojia na Elimu ya Juu (STHEP) uliotekelezwa kwa
ushirikiano wa Serikali na Bank ya Dunia, Utakavyoongeza ufanisi wa chuo
hicho,Kulia ni Msimamizi wa Mradi wa Bank ya Dunia unaotekelezwa katika
chuo hicho Bw. Shaaban Mbogo.
Mratibu
wa Mradi wa Sayansi,Teknolojia na Elimu ya Juu (STHEP) kitaifa Dkt.
Keneth Hosea (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo
pichani)jinisi mradi huo utakavyo wanufaisha walimu wa shule za
sekondari wenye shahada wanaofundisha masomo ya sekondari.Kulia ni
Msimamizi wa Mradi wa Bank ya Dunia unaotekelezwa katika chuo hicho Bw.
Shaaban Mbogo.
Mhandisi
John Kapuku akiwaonesha waandishi wa habari(hawapo pichani)Jengo la
Sayansi ya Majini na Teknolojia ambayo ni moja ya jengo linalotokana na
mradi huo unaofadhiliwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na Bank
ya Dunia lililogharimu bilioni 4.3.
Jengo
la Urithi wa Utamaduni linalotokana na mradi huo unaofadhiliwa kwa
ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na Bank ya Dunia lililogharimu
bilioni 2.6
JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU
Katika kukabiliana na changamoto zinazoikabili Elimu ya Juu nchini, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inatekeleza Mradi wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu (Science
Technology and Higher Education Project – STHEP) ambao unafadhiliwa na
Benki ya Dunia. Mradi huu umejikita katika nyanja kuu 4 ambazo ni:
kuboresha rasilimali watu kwa kutoa mafunzo ya muda mrefu na muda mfupi
(staff development), kujenga, kupanua na kukarabati vyumba vya
mihadhara, maktaba, maabara na karakana (Civil Works), kununua vifaa
vya kufundishia vikiwemo vifaa vya maabara na TEHAMA, vitabu na magari
(Procurement of Goods) na kuboresha mitaala, sera na usimamizi kwa
kutumia wataalamu washauri (Consultancy services for curriculum review,
policy, capacity building, design and supervision of civil works).
Taasisi
15 za umma zinazotekeleza mradi huu ni Chuo Kikuu Huria cha Tanzania
(OUT), Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU), Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA),
Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Chuo Kikuu Kishiriki cha
Ualimu Dar es Salaam (DUCE), Chuo Kikuu Kishiriki cha Ualimu Mkwawa
(MUCE), Chuo Kikuu cha Dares Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha Serikali cha
Zanzibar (SUZA).
Taasisi
nyingine ni Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Tume ya Vyuo Vikuu
(TCU), Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), Mamlaka ya Elimu
Tanzania (TEA), Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB),
Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia (MCST) na Wizara ya Elimu
na Mafunzo ya Ufundi.
Hadi
sasa Mradi umegharamia mafunzo ya muda mrefu kwa watumishi 191 wa
taasisi za umma masomo ya Shahada ya Uzamivu (PHD) na watumishi 208
wamepata ufadhiri wa mafunzo ya Shahada za Uzamili (Masters) katika fani
za sayansi, teknolojia na ualimu. Aslilimia 30 ya watumishi hawa
wanasomeshwa katika vyuo vikuu bora katika nchi zilizoendelea ikiwemo
Uingereza, asilimia 30 wanasomeshwa katika nchi zinazoendelea mfano
Afrika Kusini na kwingineko na waliobaki (asilimia 40) wanasomeshwa hapa
nchini. Asilimia 15 ya watumishi wanaosomeshwa na mradi huu
wamekamilisha masomo yao na wengine watamaliza mwishoni mwa mwaka huu.
Vilevile watumishi 467 wamesomeshwa mafunzo maalum ya muda mfupi.
Aidha,
mradi umejenga jumla ya majengo 25 ya mihadhara, maktaba, ofisi na
karakana ambapo mengi yapo kwenye hatua za mwisho kukamilika katika
taasisi mbalimbali.
Majengo
haya yatatumiwa na jumla ya wanafunzi 36,344 wa elimu ya juu na
wakufunzi na wahadhiri 1,640 katika taasisi za ARU, DUCE, DIT, OUT,
MUCE, SUA na UDSM.
Mradi
huu pia umenunua vifaa vya kufundishia na kujifunzia vikiwemo vifaa vya
maabara, vifaa vya TEHAMA 1,831, vitabu 4,598, mitambo ya kufundishia
na magari 19.
Mradi wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu
umesaidia Tume ya Vyuo Vikuu kujenga uwezo wa TEHAMA na kuwezesha
kudahili wanafunzi wote wanaojiunga na elimu ya juu kwa pamoja (Central
Admissions System – CAS) na umeiwezesha TCU kutoa mwongozo wa ubora wa
Vyuo Vikuu hapa nchini (Universities Standards and Benchmarks).
Aidha,
mradi umewezesha Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kuandaa
miundombinu ya TEHAMA ili waombaji wa mikopo ya Elimu ya juu waombe kwa
kutumia mtandao (Online Loan Application System – OLAS).
Mradi wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu
pia umesaidia TCU kujenga uwezo wa kukokotoa ada elekezi kwaajili ya
wanafunzi wa elimu ya juu (Higher Education Students Unit Cost).
Mradi wa STHEP ni wa muda wa miaka 7 ukiwa na duru mbili ziitwazo Adaptable Lending Program-1 (APL-1) na Adaptable Lending Program–II (APL-II). Duru ya kwanza ilianza Julai 2008.
Duru ya pili inatazamiwa kuanza kabla ya duru ya kwanza kuisha hapo Desemba, 2013 na kukamilika June, 2016.
Mradi huu unalenga kuongeza matumizi ya taaluma katika shughuli za kiuchumi nchini (application of knowledge in economic activities), na malengo ya haraka (immediate goal) yakiwa
ni kuongeza idadi ya wanafunzi na kuboresha mazingira ya kufundishia
katika elimu ya juu hapa nchini kipaumbele kikiwa katika fani za
sayansi,teknolojia na ualimu.
Ntambi Bunyazu
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
20/09/2013
Post a Comment