Akiongea na ITV, mkuu wa upelelezi wa makosa ya
jinai RCO Joseph Konyo amesema kuwa baba wa familia hiyo aliyejulikana
kwa jina la Jonas Lulinga anaekadiriwa kuwa na umri wa miaka 44
ameuawa kwa kuchinjwa na kisu huku mkewe na mtoto wao mchanga
wakiuawa kwa kunyongwa na waya wa umeme...
Tukio hilo linadaiwa
kutekelezwa majira ya saa nane usiku na mtu mmoja ambaye
walimkaribisha na kuishi nae kwa siku
nne....
Binti mmoja
aliyesalimika anasimulia tukio hilo kwa kina katika video iliyopachikwa
hapo chini.
on Sunday, September 22, 2013
Post a Comment