Mahmoud Ahmad Arusha
BUNGE la nchi wanachama wa jumuia ya maendekleo kusini mwa afrika SADC-PF, limesema kuwa limepata mafanikio makubwa katika kujenga demokrasia ,uwazi na utawala bora tangia kuanzishwa kwake mwaka 1997 .
BUNGE la nchi wanachama wa jumuia ya maendekleo kusini mwa afrika SADC-PF, limesema kuwa limepata mafanikio makubwa katika kujenga demokrasia ,uwazi na utawala bora tangia kuanzishwa kwake mwaka 1997 .
Spika
wa Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania, Anne Makinda, akizungumza
na vyombo vya habari mjini Arusha katika kikao cha kamati ya maandalizi
ya mkutano mkuu wa 34 wa jukwaa la mabunge ya jumuia ya maendeleo
kusini mwa Afrika,SADC-PF, utakaofanyika Arusha kuamnzia june 16 hadi 24
mwaka huu..
Makinda
amesema katika mkataba wa kuanzishwa kwa bunge hilo wakuu wa nchi
wanachama walisaini mkataba wa makubaliano ya kukuza demokrasia,uwazi
na utawala bora ambapo nchi kadhaa zimeweza kupanua demokrasia na
kufikia 30% ya wabunge wanawake na hilo ni jambo la kujivunia.
Makinda,
amesema mkutano huo utafunguliwa na makam wa rais Dakta Mohamed Ghalib
Bilal, Oktoba 20 ,utashirikisha wabunge 150 kutoka nchi wanachama na
wadau wa maendeleo kutoka taasisi za kitaifa na kimataifa ambao
watashiriki kikamilifu katika .
Amezitaja
nchi zinazounda jumuia hiyo kuwa ni Afrika kusini,Tanzania, Musumbiji,
Zimbabwe, Zambia, Namibia, Malawi, Lesotho, Angola, DRC Congo,
Seychelles Mauritius,ambapo Botswana na Swazilandi, hazitashiriki kwa
kuwa zipo kwenye mchakato wa uchaguzi mkuu.
Amesema
kauli mbiu ya mkutano huo ni vigezo vya kuendesha na kutathimini
chaguzi kwa nchi za kusini mwa afrika kauli mbiu hiyo imechaguliwa baada
ya miaka 13 kuanzia mwaka 1999 hadi 2013 kuhusu chaguzi mbalimbali
ambazo zimefanyika katika nchi wanachama na wameona kuna umuhimu wa
kuvipitia upya vigezo vya kusimamia na kutathimini mwenendo wa chaguzi
hizo.
Amesema
mjadala zaidi utajikita katika namna bora ya kuweka vigezo vya kuweka
na kuendesha na kuthimini mienendo na matokeo ya uchaguzi mkuu katika
nchi za sadc kwa lengo la kuzifanya chaguzi hizo ziwe huru haki na
uwazi zaidi.
Post a Comment