Mkuu wa wilaya ya Kilolo Bw Gelard
Guninita wa pili kulia akisoma taarifa ya miradi ya Kilolo kabla
ya kukabidhi mwenge Manispaa ya Iringa leo ,wa tatu ni mbunge wa
jimbo la Kilolo Prof Peter Msolla na mwenyekiti wa CCM Kilolo Bw Sety
Mwamoto na kati kati ni kiongozi wa mbio za mwenge Kitaifa Juma Alli
Simani
Viongozi mbali mbali ya Halmashauri
ya Manispaa ya Iringa wakisubiri kuupokea mwenge wa Uhuru ukitokea
wilaya ya Kilolo leo
Kutoka kulia Naibu meya wa Manispaa
ya Iringa Gervas Ndaki , mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta
kabati , Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Lediana Mafulu,
mwenyekiti wa CCM Iringa mjini Abed Kiponza , Mkurugenzi wa Halmashauri
ya Manispaa ya Iringa Terresia Mahongo ,mstahiki meya wa Manispaa ya
Iringa Aman Mwamwindi na mkuu wa wilaya ya Iringa Dr Leticia
Warioba wakisubiri kupokea mwenge wa Uhuru leo kutoka wilaya ya
Kilolo
Mkuu wa wilaya ya Iringa Dr
Leticia Warioba ( kulia) akipokea mwenge wa Uhuru kutoka kwa mkuu wa
wilaya ya Kilolo Bw Gelard Guninita mara baada ya mwenge huo
kumaliza mbio zake wilaya ya Kilolo na kuanza mbio zake Halmashauri
ya Manispaa ya Iringa leo
Wakati Rais Jakaya
Kikwete kesho anataraji kuzima mwenge
wa Uhuru katika
kilele cha mbio
hizo kitakachofanyika kitaifa
katika uwanja wa
samora mjini Iringa , mkimbiza mwenge
Kitaifa Christopher Emanuel amewataka
viongozi wa upinzani
wanaotaka mwenge wa Uhuru kuwekwa makumbusho kuanza wao
kupeleka familia zao
huko.
Akitoa ujumbe wa Mwenge
wa Uhuru katika chuo
cha ualimu Krellu mjini
Iringa jana Emmanuel alisema kuwa ni fikra mgando kwa kiongozi anayeitakia amani Tanzania
kutaka watanzania kuacha
kuendelea kumuenzi baba wa taifa
kwa kukimbiza mwenge huo.
Alisema kuwa suala la
kuweka mwenge makumbusho ni suala lisilo wezekana kwani mwenge
wa uhuru kila mwaka unakimbizwa
kwa ujumbe mbali mbali ikiwa ni pamoja na
kuzungumzia suala zima la amani na
utulivu nchini.
Hata hivyo alisema
kuwa kwa kiongozi ambae
anataka mwenge kuwekwa makumbusho ili
watanzania kutembelea kuuona kama sehemu ya utalii ni vema wakaanza wao kwa kupeleka
ndugu zao ama wao
wenyewe kwenda kuishi
huko ili watanzania
wakawaone wao sio mwenge wa Uhuru .
Wakati kiongozi wa mbio
hizo za mwenge wa Uhuru
Juma Alli Simai akiwataka wakazi wa Manispaa ya Iringa
kuwapuuza kwa nguvu zote wanasiasa ambao wanashindwa
kuwatumikia watanzania na
badala yake kubeza kazi nzuri iliyofanywa
na inayoendelea kufanywa na serikali
iliyopo madarakani chini ya rais Jakaya
Kikwete.
Kwa upande wake mkuu
wa mkoa wa Iringa aliwataka
wananchi wa Manispaa ya Iringa na
mkoa kwa
ujumla kujitokeza kwa wingi
katika kilele cha mbio za mwenge wa Uhuru KItaifa
katika uwanja wa Samora
na kuwa maandalizi yote ya
uzimaji wa mwenge huo yamekamilika.
Alisema kuwa mkoa
wa Iringa ambao ndio mkoa wa mwisho kwa kukimbiza mwenge huo
umemaliza mbio zake katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa
jana na leo asubuhi mwenge
huo utakabidhiwa mkoani kabla ya
mkoa kuukabidhi Taifa kwa ajili ya kuuzima .
Mkuu
huyo wa mkoa alisema kuwa asubuhi Rais Kikwete atashiriki ibada ya
kumbukumbu ya kifo cha baba wa taifa itakayofanyika kanisa la RC
Kihesa na baada ya hapo shughuli za kilele cha mbio za mwenge na
wiki ya vijana zitafanyika katika uwanja wa Samora .
Mwenge wa Uhuru ukiwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa
umezindua jumla ya miradi
8 yenye thamani ya zaidi ya Tsh milioni 940.2
MWISHO
credit: matukio daima blog
Post a Comment