WATANZANIA
wametakiwa kumuenzi Baba wa Taifa, hayati Mwalimu JK. Nyerere kwa
kuchukia vitendo vya uhalifu na wahalifu vinavyotokea katika jamii ili
kuhakikisha taifa la Tanzania linaendelea kuwa la amani, Usalama na
utulivu kuanzia ngazi ya familia hadi Taifa.
Hayo
yalibainishwa na Msemaji wa Jeshi la Polisi, Mrakibu Mwandamizi wa
Polisi (SSP) Advera Senso wakati akijibu swali lililomtaka yeye kama
mwanausalama anataka watanzania wamuenzi namna gani muasisi wa taifa la
Tanzania kwani yeye alikuwa ni kiongozi wa amani kwa Tanzania na
Afrika kwa ujumla.
Akimzungumzia
Baba wa Taifa, Senso alisema kuwa Mwalimu Nyerere alikuwa kiongozi
mwenye msimamo imara, alikuwa anachukia vitendo vya vyote vya
ubadhilifu, unyanyasaji, uchochezi wa kidini, kisiasa ikiwa ni pamoja
na vitendo vya uhalifu, vitu ambavyo ni hatari kwa taifa linalohitaji
ushirikiano wa pamoja baina ya Serikali na wananchi wake ili liweze
kujikwamua kimaendeleo hususani kiuchumi, kisisasa yakiwemo maendeleo ya
kiulinzi na usalama.
Alibainisha
kuwa, miongoni mwa mbinu za kupata maendeleo ya kiusalama ni
ushirikiano wa jamii katika kubaini na kufichua uhalifu na wahalifu
katika makazi yao kwa kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi au kushirikiana
na askari tarafa waliokwisha sambazwa katika tarafa kote nchini ili
kushirikiana na familia katika kutatua kero za kiusalama zinazowakabili.
“familia
zikiwa salama, tutakuwa na mtaa salama, Mitaa ikiwa salama, tutakuwa na
kata salama, Kata zikiwa salama tutakuwa na tarafa salama, Tarafa
zikiwa salama tutakuwa na Wilaya salama, Wilaya zikiwa salama, tutakuwa
na Mikoa salama, Mikoa ikiwa salama, Tutakuwa na Taifa salama” alisema
Senso.
Pia
alitoa wito kwa wananchi kutowaonea haya wahalifu badala yake waendelee
kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu kwa kuwa kosa la jinai huwa
halifutiki, taarifa hizo ni muhimu kwani zitasaidia kukamatwa kwa
wahalifu waliotenda uhalifu katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Aliongeza
kuwa mhalifu ni adui namba moja wa maendeleo ya wananchi na taifa kwa
ujumla kwani unyang’anya au kuiba mali za mtu au umma ambazo
zimepatikana kwa taabu, jambo ambalo hata baba wa taifa alikuwa
akilikemea kwani linarudisha nyuma maendeleo.
Post a Comment