Viongozi
wa Tanzania ukisikiliza kwa makini uongozi wa MCC hawapo pichani wakati
wa majadiliano. Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Jamhuri
ya Muungano Dkt. Servacius Likwelile, Balozi wa Tanzania Marekani na
Mexico Mhe. Liberata Mulamula, Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano
Mhe. Dkt. Wiliam Mgimwa, Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe. Yusuph Mzee, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Zanzibar Bw. Khamis Mussa.
Ujumbe wa Tanzania wakifuatilia majadiliano na MCC mjini Washington, kutoka kulia ni Kamishna
wa Fedha za Nje Jamhuri ya Muungano Bw. Said Magonya, Kamishna wa Fedha
za Nje Zanzibar, Bi. Bihindi Nassor, Naibu Ganana wa BOT Dkt. Natu
Mwamba pamoja na Mkurugenzi wa Mipango Zanzibar.
Ujumbe wa Tanzania na Viongozi wa MCC katika majadiliano
Picha zote na Bi. Ingiahedi Mduma na Bi Eva Valerian – Washington DC
…………………………………………………………………………………………………
Wakati
Mikutano ya mwaka ya Shirika la fedha la kimataifa na makundi ya benki
ya Dunia ikiendelea hapa mjini Washington DC, Ujumbe kutoka Tanzania
watumia nafasi hiyo kukutana na Uongozi wa Millenium Challenge
Corporation (MCC) kwa madhumuni ya kujadili mafanikio
yaliyopatikana kutokana na shirika hili la Marekani. MCC awamu ya kwanza
ilisaidia sana miradi mbalimabli Tanzania, ambapo walitoa dola milioni
698 ambayo ilielekezwa katika miradi ya barabara, umeme, maji pamoja na
miradi ya barabara Zanzibar pamoja na uwanja wa ndege wa Mafia (Mafia
Airport).
Akizungumza
na vyombo vya Habari mjini hapa, Waziri wa Fedha Dkt. Wiliam Mgimwa
alisema kuwa “Miradi hiyo yote ya MCC ya kwanza ilikwenda vizuri sana na
tunamaliza nao mkataba tukiwa tumefanikiwa sana katika ujenzi wa miradi
hiyo”.
Aidha
Mgimwa aliendelea kutoa ufafanuzi akisema kuwa “lengo kubwa la kukutana
na Uongozi wa MCC ni kuangalia mafanikio yaliyopatikana katika miradi
waliyoianzisha na ni nini tumejifunza kutoka katika hiyo miradi ili
tuepuke matatizo katika miradi mingine inayofuata”.
Katika
majadiliano hayo ujumbe wa Tanzania ulipata fursa ya kuzungumzia miradi
ya MCC ya awamu ya pili ambapo MCC wamekubali kuisaidia Tanzania
kueneza umeme vijijini hasa vijiji vikubwa vinavyozalisha mazao kwa
wingi na vijiji vyenye watu wengi pamoja na kujenga barabara katika maeneo ya uzalishaji.
“Hii
itakuwa nafasi ya Tanzania kuweza kusaidia kueneza umeme vijijini
ambapo wananchi wetu watapata nafasi ya kutumia umeme huo katika miradi
midogo midogo na vile vile kwa ajili ya kuhakikisha kuwa miradi ya
barabara hasa katika vijiji vinavyozalisha mazao wanaweza kupokea
pembejeo na baada ya kuvuna kuweza kufikisha mazao yao kwa walaji.”
Alifafanua Mgimwa.
Hali ya hewa ya mjini hapa ni baridi kiasi na manyunyu ya hapa na pale.
Imetolewa na:
Ingiahedi Mduma
Msemaji Mkuu
Wizara ya Fedha
Washington D.C
Post a Comment