Wahamiaji
haramu 16 kutoka nchini somalia wamekamatwa Mkoani morogoro wakiwa
wamejificha katika lori la mizigo lililosheni chokaa likitokea jijini
dar es salaam kuelekea mkoani mbeya Kupatikana kwa wahamiaji haramu hao
kunatokana na ushirikiano wa wananchi ambao umesaidia kukamatwa kwa
wahamiaji hao huku wakidai kuwa baadhi yao walikosa hewa kufuatia
kujificha katika mizigo hiyo Kwa upande wake afisa uhamiaji
mkoa wa Morogoro Hamprey Minja amesema kuwa dereva wa gari
hilo amekamatwa na kufikishwa kituo cha polisi ambapo amesema kuwa
vyombo vya ulinzi na usalama vimedhibiti kwa kiasi kikubwa maeneo ya
mipaka kwa ajili ya kudhibiti matukio ya wahamiaji haramu hali
inayopelekea wahamiaji hao kutumia njia nyingine ikiwemo ya kujificha
katika magari ya mizigo.
Loading...
Home » Unlabelled » WAHAMIAJI HARAMU 16 WA SOMALIA WAKAMATWA NDANI YA LORI LILILOBEBA CHOKAA MKOANI MOROGORO
Post a Comment