Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WAKAZI DODOMA WAANDAMANA KUPINGA BOMOABOMOA YA CDA

 


 Maelfu ya Wananchi wa Kata ya kikuyu kusini wakiandamana katika mitaa ya mji wa Dodoma kwa ajili ya kupinga kubomolewa na mamraka ya ustawishaji makao makuu  [CDA] wanaotarajia kubomoa nyumba, mapagale na misingi ya wakazi hao.
  Maelfu ya Wananchi wa Kata ya kikuyu kusini wakiandamana katika mitaa ya mji wa Dodoma kwa ajili ya kupinga kubomolewa na mamraka ya ustawishaji makao makuu  [CDA] wanaotarajia kubomoa nyumba, mapagale na misingi ya wakazi hao.
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akipaza sauti ya matumaini kwa wakazi wa Kata ya kikuyu kusini walioandamana kupinga Bomoabomoa ya CDA waliokuwa wamepanga kubomoa nyumba na misingi katika eneo hilo.
Diwani wa kata ya Kikiyu kusini Ancelmu Kutaka akifafanua jambo mbele ya Wananchi wa kata hiyo waliondamana kupinga kubomolewa na Mamraka ya ustawishaji makao makuu [CDA] walipanga kuboa wakati wowote kuanzia leo.
Kaimu Mkurugenzi wa CDA Paskas Mulagili Akifafanua jambo wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali kuhusu maandamano ya wananchi wa kata ya Kikuyu Kusini walioandamana kupinga ubomoaji unaotarajiwa kufanywa na mamlaka hiyo siku yoyote kuanzia leo. PICHA NA JOHN BANDA

Na John Banda, Dodoma
WAKAZI wa Kata za Kikuyu Kusini na Kilimani mkoani Dodoma wameandamana kupinga amri iliyotolewa na Mamlaka ya Ustawishaji ya Makao Makuu (CDA) ambayo inawataka kuhama katika eneo hilo ndani ya siku saba.
Wakazi hao walioandamana kutoka Kikuyu hadi Viwanja vya Nyerere Square katikati ya mji wakimtaka mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi kuzungumza nao.
Maandamano hayo yalisindikizwa na ulinzi wa polisi hadi katika viwanja hivyo huku wakazi hao wakiwa wameshikilia mabango yenye jumbe mbalimbali.
Wakazi hao wakiwa wanaimba nyimbo huku wakiinua mabango yao juu yenye ujumbe kama Cda ni zaidi ya Alshababi, CCM mnaiona bomoabomoa, Cda ni zaidi ya Nduli Idd Aminini Dada na lingine likisomeka Hata wanyama hupewa hifadhi.
Wakizunguza na waandishi wa habari katika viwanja hivyo wakati wakimsubiri mkuu wa mkoa baadhi ya wananchi na viongozi wao wa mitaa walidai kuwa lengo la maandamano hayo ni kufikisha kilio chao kwa serikali ya mkoa.
Andrew Mdumi mwenyekiti wa mtaa wa Mkalama ambao ni sehemu ya eneo linalotakiwa kuvunjwa alisema kuwa wameamua kufanya maandamano hayo mara baada ya kupewa amri ya kuondoka katika eneo wanaloishi kwa kipindi kirefu.
Mdumi alisema, kuwa Mamlaka ya ustawishi Makao makuu imekuwa ikiwapatia namba kila wakati na kudai kuwa itakuja kuwapimia lakini katika hali ya kushangaza imewapa amri ya kuondoka ndani ya siku saba kwa madai kuwa wamevamia katika eneo hilo ambalo lilikuwewa limetengwa kwajili ya bustani za mbogamboga na matunda.
“Wanataka tuondoke ili kupisha kilimo cha mbogamboga na matunda hivi kweli mboga na maisha yetu kipi cha msingi kuna nyumba zaidi ya 1000 ambazo watakakuzibomoa kwajili tuu ya kupisha bustani” alisema
Alisema kuwa wamekuwa wakishirikiana na CDA kwa kipindi kirefu ili kuweza kufanikisha zoezi la upimaji wa viwanja hivyo hata kwa gharama zao wenyewe.
Mwekiti wa kamati ya upimaji katika Kata ya Kikuyu kusini Mathew Ndallu, alisema kuwa katika kufuatilia suala hilo la kupimiwa viwanja walikutana na CDA na kukubaliana kuwa waje wafanye utambuzi wa nyumba zilizopo, mapagale na misingi ili waweze kufanya upimaji.
Ndallu alisema kuwa walikubaliana na kuwa kutokana na eneo hilo kuwa halijapimwa wao wako tayari kuchangia gharama za upimaji ili kuwezesha zoezi hilo kufanyika.
“Tulikubaliana nao mara baada ya wao kuja kutambua idadi ya nyumba mapagale na misingi watupimia na sisi tuko tayari kuchangia kiasi cha sh.500,000 kwa kila mwenye eneo” alisema Ndalllu.
Aidha alisema kuwa katika hali ya kushangaza pale ambapo walikuwa wanasubiri kupimiwa CDA waliwageuka na kuwataka kwanza wao wapatiwe viwanaja 500 ili waweze kuwapiamia.
“Mara baada ya kukubaliana nao kuwa tuko tayari kuchangia lakini Mkurugenzi alituambia kwanza tuwape wao viwanja 500 ili waweze kuja kutupimia na kama hatutakubali basi watakuja kutubomolea” alisema.
Alisema kuwa mara baada ya wao kukataa kumpa mkurugenzi huyo viwanja hivyo aliwaandikia barua hiyo ambayo ilikuwa inawataka wakazi wa maeneo hayo kuondoka kabla ya tarehe 30 ya mwezi Septemba (jana).
“Walituandikia barua ambayo inatutaka kuaondoka ndani ya siku hizo saba ikiwa ni kuanzia tarehe 23 ya mwezi huu ambapo inaishia leo (jana) na kesho (leo )wanakuja kuanza kubomoa” alisema Ndallu.
Alisema kutokana na hali hiyo ambayo imeonyesha kuwa CDA imeshindwa kuwasikiliza kilio chao wameona kuwa hiyo ndiyo njia sahihi ya wao kupata suluhu ya tatizo lao.
Alisema kuwa jumla ya mitaa mnne katika kata hizo ndiyo inayotakiwa kubomolewa ambayo ni mitaa ya Mkalama, Chidachi pamoja na Image A na B.
Akizungumza na kundi la wakazi hao mkuu wa mkoa wa Dodoma Dk Rehema Nchimbi, alisema kuwa anatengua amri hiyo iliyotolewa na CDA na kumtaka Mkurunzi wa mamlaka hiyo kukutana na viongozi wa maeneo husika.
“Naitengua amri hiyo na namwagiza Mkurugenzi akutane na wananchi hawa pamoja na viongozi wao ili kuweza kufikia muafaka kwani kubomoa sio suluhu hamuwezi kubomoa Dodoma nzima na ningependa kuletewa taarifa juu ya sula hili … mnachotakiwa ni kuboresha na kutumia njia sahihi ambazo hazita waumiza wananchi ambao ndiyo wateja wenu.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top