Mwenyekiti
wa Muungano wa Jinsia na Katiba (GFC) , Magdalena Rwebangira
akiwasilisha mada wakati Warsha ya mrejesho na taarifa kwa wadau kutoka
Jukwaa la Katiba ya siku moja iliofanyika Septemba 3o-2013 katika ukumbi
wa Karimjee jijini Dar es salaam, lengo likiwa ni kujadili rasimu ya
Katiba na baadhi ya mambo yaliyojadiliwa ni haki ya kumiliki mali na
kutaka Katiba iwe na kipengele kinachohusu haki sawa ya kumiliki ardhi
kwa wanawake, watoto na makundi mengine maalum, ilioandaliwa na Chama
cha Wanasheria Wanawake Tanzania TAWLA Mbunge
wa viti maalumu Ester Bulaya (CCM, akichangia mada wakati wa Warsha ya
wadau wa Jukwaa la katiba yasiku moja iliofanyika Septemba 3o-2013
katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam.Mbunge
wa viti maalumu, Ester Matiku (kulia) Mbunge wa viti maalumu, Ester
Bulaya (CCM, (kushoto kwake) akiwa pamoja na Wabunge wengine
walioudhuria,wakiwa kwenye Warsha ya mrejesho na taarifa kwa wadau
kutoka Jukwaa la Katiba yasiku moja iliofanyika Septemba 3o-2013 katika
ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam,lengo la Warsha hiyo ilikuwa
kujadili rasimu ya Katiba na baadhi ya mambo yaliyojadiliwa ni haki ya
kumiliki mali na kutaka Katiba iwe na kipengele kinachohusu haki sawa ya
kumiliki ardhi kwa wanawake, watoto na makundi mengine
maalum,ilioandaliwa na Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania TAWLA
…………………………………………………………………………………………………
Na Philemon Solomon wa Fullshangwe , Dar es Salaam
CHAMA
cha wanasheria wanawake Tanzania (Tawla) na Wanaharakati pamoja na
wabunge Wanawake wamewataka wananchi kutengeneza Katiba ya Watanzania
wote na si kuegemea katika vyama au taasisi fulani pamoja na kuwa na
Katiba ya inayomlinda kila mtu sanjari na kutoa mapendekezo yao.
Hayo
yalizungumzwa Jijini Dare s Salaam Septemba 30-2013, na Mwenyekiti wa
Muungano wa Jinsia na Katiba (GFC) Magdalena Rwebangira wakati
walipokuwa wakifanya mrejesho wa taarifa kwa wadau kutoka Jukwaa la
muungano wa jinsia na Katiba kwa lengo la kuhakikisha inapatikana Katiba
bora kwa maslahi ya Taifa na wananchi kwa ujumla.
“Mimi
ni mwanasheria lakini itafika wakati nitastaafu na sitaweza kufanya
hizo kazi hivyo siwezi kutetea eti mwanasheria apewe kitu fulani au upo
katika chama fulani halafu utete mpewe/kipewe kitu fulani, hivyo
natamani kuweka ukurasa mpya ili kupata katiba nzuri iliyobora kwa
maslahi ya taifa, alisema.
Katika
warsha hiyo watu mbalimbali wakutanishwa wakiwemo wabunge na baadhi ya
wananchi kutoka taasisi mbalimbali kwa lengo la kujadili rasimu hiyo ya
Katiba na baadhi ya mambo yaliyojadiliwa ni haki ya kumiliki mali na
kutaka Katiba iwe na kipengele kinachohusu haki sawa ya kumiliki ardhi
kwa wanawake, watoto na makundi mengine maalum.
Pia
walijadili haki ya usawa na utambuzi wa katiba kama sheria mama iliyo
juu ya sheria zote na kutaka iwe na kipengele kinachobatilisha sheria
zote za ubaguzi wa kijinsia sanjari na kuwepo kwa kipengele kinacholinda
haki na utu wa mwanamke kwa kukataza masuala unyanyasaji na ukatili wa
kijinsia, ubaguzi kwa misingi ya dini, uraia, rangi, au hali ya ndoa.
Pia
wadau hao walijadili suala la uwakilishi na kuitaka Katiba mpya iwe na
kipengele kinachaonisha wazi kuwa nafasi za juu ya uongozi wa nchi ziwe
na uwino kwa wanawake na wanaume kwa maana rais akiwa Mwanaume Makamu
wake au Waziri Mkuu awe mwanamke.
Mbunge
wa viti maalumu Ester Bulaya (CCM) mkoani Mara amewataka wabaunge
kuunganisha nguvu zao katika kukaa pamoja na kutengeneza katiba Mpya na
si kuanza kuyumbisha hali itakayowapa nafasi watu wa nchi ya jirani
kupenyeza hila zao na kuiweka nchi pabaya kwa maslahi yao.
“Ili
kupata Tanzania iliyosafi kwa miaka ijayo ni vema wabunge wote
tukaonganisha nguvu zetu na kuwa kitu kimoja kabla ya kwenda katika
bunge la Katiba kwa lengo la kuwa na masahisho sahihi kwa maslahi ya
taifa na si kutegeana na kwenda kukomoana katika Bunge,” alisema.
Post a Comment