Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt Abdallah Kigoda, ambaye pia ni Mbunge wa Handeni.
Na Mashaka Mhando, Handeni
MBUNGE
wa Handeni Dkt Abdallah Kigoda, ameaahidi kushirikiana na kuwasaidia
waandaaji wa Tamasha la Utamaduni na Michezo lililopewa jina la ‘Handeni
Kwetu’ litakalofanyika Desemba 14 mwaka huu mjini Handeni,
mkoani Tanga, ili kuunga mkono jitihada za wadau katika suala zima la
utamaduni na maendeleo.
Akizungumza
wakati akizindua kisima cha maji katika soko la zamani lililopo katika
mji wa Chanika, Dkt Kigoda, alisema anaunga mkono tamasha hilo ambalo
litaibua fikra na mtizamo mpya wa utamaduni miongoni mwa wananchi
wilayani hapa.
“Waandaji
wa Tamasha la Utamaduni wamenipa taarifa za kufanyika tamasha hilo nami
kama mbunge wa jimbo hili sina budi kuwaunga mkono kufanikisha tamasha
hilo na nitashirikiana nao,” alisema Dkt Kigoda ambaye pia ni Waziri wa
Viwanda, Biashara na Masoko.
Dkt
Kigoda alisema suala la utamaduni ni suala mtambuka ambalo linagusa
mioyo ya wananchi wengi hivyo unapoweka tamasha kwa ajili ya utamaduni
wa ngomalicha ya kuwapa burudani wananchi hutoa hamasa kwa vijana
kupenda mila na utamaduni hasa suala na ngoma za asili.
Mbunge
huyo alitoa wito kwa wananchi wilayani humo na wale waliopo nje ya
handeni kujitokeza kushiriki tamasha hilo ili kuibua mawazo mapya juu ya
masuala ya utamaduni na michezo yaliyokosa msisiko kutokana na kutopewa
kipaumbele.
Mbunge huyo, aliahidi kusaidia tamasha hilo baada ya kupewa taarifa na mwandaaji wake Kambi Mbwana.
Wadhamini
waliothibitisha kushiriki katika tamasha hilo ni pamoja na Phed Trans
inayomilikiwa na Yusuphed Mhandeni, Grace Products, Screen Masters,
Dullah Tiles $ Construction Ltd, Katomu Solar Specialist na Country
Business Directory (CBD) na Michuzi Media Group.
Wengine
ni duka la mavazi la Chichi Local Ware, SmartMind & Partners chini
ya ANESA COMPANY LIMITED, ikidhamini kwa kupitia kitabu cha ‘NI WAKATI
WAKO WA KUNG'AA, Screen Masters, Saluti5.com, Lukaza Blog, Kajunason
Blog, Jiachie Blog na Taifa Letu Blog.
Katika
hatua nyingine, mbunge huyo alisema kuwa wataalamu wanafanya utafiti
kwa ajili ya kuchimba kisima katika uwanja wa mpira wa Azimio ambao
unakarabatiwa ili uweze kutumika kwa michezo ya Ligi Kuu na klabu ya
Mgambo JKT.
Alisema
tayari ametoa kiasi cha shilingi milioni 250 kutoka katika mfuko wake
wa maendeleo ya jimbo ili kuukarabati uwanja huo ambao tayari umeoteshwa
nyasi mpya na kujengwa vyumba vya kubadilishia ngu wachezaji pamoja na
jukwaa kuu.
Post a Comment