TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Emmanuel Nchimbi ameunda Kikosi Kazi kitakachokuwa na jukumu la Kuratibu na Kusimamia Ukomeshwaji wa Vitendo vya mauaji ya Wazee, yanayotokea mara kwa mara katika maeneo ya Kanda ya Ziwa hapa nchini.
Kuundwa kwa Kikosi Kazi hicho kunatokana na kukithiri kwa ongezeko la matukio ya mauaji ya wazee, yanayotokana na imani za kishirikina yanayotokea katika baadhi ya Mikoa ya Tanzania Bara hususani Kanda ya Ziwa ambayo yamekuwa yakisababisha madhara makubwa katika jamii ya Watanzania.
Miongoni mwa madhara hayo ni pamoja na Watu kufariki dunia hususani wazee, Matukio hayo kuendelea kuacha makovu
ya chuki na hisia za
kulipiza kisasi, Matumizi ya ziada ya rasilimali katika kuimarisha miundo
mbinu ya ulinzi na usalama, ikiwemo pia Nchi kupoteza sifa ya kuwa kisiwa cha
amani.
Kikosi Kazi hicho chenye wajumbe kumi (10) ambacho kimeanza kazi tangu Oktoba Mosi mwaka huu kinaongozwa na Mwenyekiti wake Naibu Kamishna wa Polisi Ernest Mangu ambaye pia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza.
Wajumbe wengine wa Kikosi Kazi hicho ni pamoja na Kamishna Msaidizi wa Polisi Leornard Paul ambaye ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita,Kamishna Msaidizi wa Polisi Salum Msangi ambaye ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu,Kamishna Msaidizi wa Polisi Peter Ouma ambaye ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora.
Wajumbe wengine kutoka vyombo vya ulinzi na usalama ni pamoja na Jacob Mutashongerwa, Gaston Peter Ndwata, Fulcon Nguli, Roman Matemu, na Anna Tegullo.
Hatua ya kuundwa kwa Kikosi Kazi hicho, kitakachofanya kazi kwa muda wa miezi sita ni Mkakati wa Serikali kupitia Jeshi la Polisi kushughulikia ukomeshwaji wa tatizo la mauaji ya wazee yanayotokea hasa katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiwemo Mwanza, Shinyanga, Geita, Simiyu na Tabora.
Lengo la kuundwa kwa Kikosi Kazi hicho ni kutafuta njia mbadala za kukomesha mifumo ya kijamii inayoweka imani za kishirikina zinazosababisha mauaji katika umri wa wazee ambao wanahitaji kuishi kama raia wengine.
Kikosi kazi hiki kitakuwa na jukumu la kuhakikisha kuwa njia zitakazotumika kukomesha mifumo ya kijamii inayochangia kasi ya kuongezeka kwa mauaji ya wazee zinabadilisha mtazamo hasi wa jamii ambayo badala ya kuwaenzi wazee imegeuka kwa kuwatuhumu kuwa ni watu wabaya na hawafai kuishi na hatimaye kuwaua kikatili kwa visingizio vya imani za kishirikina.Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI,
11Oktoba, 2013

Post a Comment