ZAIDI
ya Wanawake 8,700 hufariki duni kila mwaka nchini Tanzania kutokana na
matatizo ya ujauzito na hasa wakati wa kujifungua. Takwimu hizi
zinaonesha takribani wanawake 24 hupoteza maisha kila siku huku
ikikadiriwa mmoja kufa kila baada ya saa moja.
Hata
hivyo wataalamu wa afya wanasema moja kati ya sababu zinazochangia vifo
hivi ni kukosekana kwa huduma za dharura katika Vituo vya Afya wakati
wa kujifungua. Hata hivyo Serikali ya Tanzania mwaka uliopita katika
ahadi zake imeahidi kupunguza vifo hivi kwa asilimia 50 ifikapo mwaka
2015.
“Si
sahihi mama mjamzito kufa wakati wa kujifungua au si sahihi mama huyu
kupoteza uhai wake kwa kuugawa kwa kiumbe anachokileta duniani, hii
haiwezi kukubalika. Na inasikitisha zaidi pale maisha ya mama huyu
yanapotea hata kwa mambo ambayo yanaweza kuzuilika,” anasema Rais
Kikwete katika hotuba yake mbele ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (U.N) Ban Ki-moon.
Wewe
pia unaweza kushiriki katika kupigania kutokomeza vifo hivi kwa akina
mama wajawazito pamoja na watoto. Je, unataka kushiriki? Tafadhali fuata
kielelezo/link hii hapa chini:-
Post a Comment