Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiangalia kifaa kipya
kabisa cha mawasiliano ya kompyuta Maarufu ipad kwenye kampuni ya
Microsoft akishuhudiwa na Waziri wa Biashara Kushoto yake Mh. Nassor
Ahmed Mazrui.
Kulia yake ni Mtaa lamu wa Kompyuta wa Kampuni ya Maicrosoft Mhandisi
Daniel Moloznk na Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha
Suleiman Iddi.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kati kati
akibadilishana mawazo na Mawaziri wake aliofuatanao nao katika ziara yao
Nchini Marekani. Kushoto yake ni Mh. Nassor Ahmed Mazrui Waziri wa
Biashara, Viwanda na Masoko na kulia yake Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohammed Aboud Mohammed.
Balozi
Seif akiagana na Naibu Mkurugenzi wa Mfuko wa Kimataifa wa Misaada wa
Bill na Melinda Gates Bibi Arlene Mitchell mara baada yha mazungumzo yao
katika Ofisi ya Mfuko huo zilizopo kati kati ya Jiji la Seattle.
Kati kati yao ni Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Mh. Nassor Ahmed
Mazrui.
Balozi
Seif akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Mfuko wa Kimataifa wa
misaada wa Bill na Melinda Gates pamoja na ujumbe aliofuatana nao mara
baada ya mazungumzo yao kwenye ofisi ya Mfuko huo Mjini Seattle.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Znzibar Balozi Seif na Ujumbe wake wakiwa katika
picha ya pamoja kabla ya kuanza kutembelea ofisi ya Kampuni ya Microsoft
kati kati ya Mji wa Seattle – Washing Nchini Marekani.
Rais
wa Chama cha Wafanyabiashara, wenye Viwanda na Wakulima Zanzibar Bw.
Abdulla Abass akimpatia zawadi Maalum za Zanzibar Mkurugenzi Mkuu wa
kitengo cha Elimu ya Afya cha Microsoft Bwana Bill Crounse Mjini
Seattle.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif na ujumbe wake akiangalia
baadhi ya kompyuta mpya zilizoingia kwenye soko katika ofisi za Kampuni
ya Kimataifa bya Microsoft Mjini Seattle – Washington Nchini Marekani.
Picha na Hassan Issa wa –OMPR – ZNZ.
Jamii
popote pale Duniani inaweza kuendelea kuishi kwa amani, furaha na afya
iwapo Wananchi wenyewe kwa kuzishirikisha Taasisi na mashirika
yaliyowazunguuka watazingatia zaidi umuhimu wa taaluma ya kinga badala
ya kusubiri tiba.
Kauli
hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa kitengo cha huduma za Afya cha
Kampuni ya Kimataifa ya mitandao ya Mawasiliano ya Kompyuta ya Microsoft
Bwana Bill Crounse wakati akizungumza na Ujumbe wa Zanzibar unaoongozwa
na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ambao uko
Nchini Marekani kwa ziara ya wiki moja ya Kiserikali.
Bwana
Crounse alisema kwamba jamii kadhaa Duniani hasa katika Nchi
zinazoendelea nyingi zikiwamo ndani ya Bara la Afrika zimekuwa
zikikabiliwa na magonjwa mbali mbali yanayoibuka kila siku kwa kukosa
elimu ya kinga.
Alisema
Kampuni ya Microsoft licha ya shughuli zake za kibiashara lakini hivi
sasa imeamua kutoa elimu ya kinga katika mataifa mbali Duniani kwa lengo
la kupunguza maradhi yanayosababisha vifo ambavyo baadhi yake vinaweza
kuwepukia.
Mkurugenzi
Mkuu huyo wa kitengo cha huduma za kinga ya Afya cha Microsoft
alieleza kwamba Taasisi hiyo katika kukabiliana na wimbi la maradhi
imejitolea kutoka elimu ya kinga ya afya kwa kupitia mitandao ya
mawasiliano ya kompyuta.
Bwana
Bill Crounse alifahamisha kuwa mpango huo tayari umeshahusisha zaidi ya
Mataifa 120 Barari Asia na Afrika akizitaja baadhi ya nchi hizo kuwa ni
pamoja na Kenya, Somalia, Msumbiji,Misri na Morocco kwa Afrika na India
na Bangladesha kwa Asia.
Akizungumzia
taaluma inayotolewa maskulini na Kampuni hiyo Mkurugenzi wa Afrika wa
Microsoft Bwana Louis Onyango Otieno alimueleza Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar Balozi Seif na Ujumbe wake kuwa Taasisi hiyo tayari
imeshafungua milango ya kutoa taaluma Barani Afrika kwa kutumia njia ya
mitandao.
Bwana
Otieno alisema elimu hiyo inayokadiriwa kufikia zaidi ya asilimia 44%
imelenga kutolewa kwa watoto wenye umri wa miaka 15 ili kuwajengea
uwezo wa kitaaluma.
Mapema
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Zanzibar Nd. Abdulla Mzee Abdulla
aliiomba Kampuni ya Microsoft kuangalia upya mikataba iliyowahi
kutiliana saini na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuendelea
kusaidia sekta ya elimu Zanzibar.
Nd.
Abdulla alisema Serikali ya Marekani kupitia Taasisi zake ikiwemo ile ya
Microsoft ziliwahi kusaidia kuanzisha mradi wa kuimarisha elimu kwa
kutumia mitandao ya kompyuta kwa skuli za msingi Unguja na Pemba.
Akitoa
shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif
aliipongeza Kampuni hiyo ya Microsoft kwa juhudi zake inazochukuwa za
kusaidia taaluma tofauti ikilenga zaidi zile nchi zinazoendelea ikiwemo
Zanzibar.
Balozi
Seif alisema misaada ya taasisi hiyo kwa kiasi kikubwa imeziwezesha
nchi changa kupiga hatua kubwa kielimu na kuiomba Kampuni hiyo kuendelea
kuiunga mkono Zanzibar katika harakati zake za kuimarisha sekta ya
elimu.
Baadaye
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif na Ujumbe wake
waliendelea na ziara yao kwa kutembelea Ofisi za Mfuko wa Kimataifa wa
misaada wa Bill na Melinda Gates zilizopo kati kati ya mji wa Seattle -
Washington.
Katika
mazungumzo yao Ofisa Mipango wa Mfuko huo Bibi Windy Wilkins alisema
Taasisi hiyo inajaribu kuangalia uwezekano wa namna ya kuisaidia
Zanzibar katika sekta ya uvuvi wa bahari kuu.
Bibi
Windy alisema hivi sasa taasisi hiyo kupitia mpango wa AGRA imepanga
kuongeza nguvu katika utoaji wa taaluma ya uzalishaji wa maziwa na
vifaranga ikilenga kuwajengea zaidi uwezo wafugaji wadogo wadogo.
Alisema
hatua hiyo imechukuliwa kutokana na wafugaji wengi kuishi vijijini
kiasi kwamba taaluma ndio njia pekee itakayowawezesha kuingia katika
soko la kimataifa litakalowapa nguvu na uwezo wa kuongeza kipato chao.
“ Kwa
kutambua kuwa kilimo ni gari ya Biashara Taasisi yetu imeamua kujipangia
kutumia Dola za Kimarekani Milioni mia Nne kwa mwaka katika miradi ya
Taaluma “. Alifafanua Bibi Windy Wilkins.
Naye
kwa upande wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliueleza
Uongozi wa Mfuko wa Misaada wa Kimataifa wa Bill na Melinda Gates
kwamba Zanzibar na Tanzania kwa ujumla muda wote imekuwa ikitilia mkazo
sekta ya Kilimo ambayo ndio uti wa mgongo wa Taifa.
Balozi
Seif alisema wananchi wengi wa Tanzania na Zanzibar wamekuwa wakiishi
katika maeneo ya mashambani kwa zaidi ya asilimia 80% idadi ambayo
inapaswa kusaidiwa kitaaluma ili izalishe kitaalamu zaidi.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliuomba Uongozi wa Mfuko wa Kimataifa wa
Misaada wa Bill na Melinda Gates kutuma Timu ya wataalamu wa sekta ya
kilimo kutembelea Zanzibar ili kuangalia maeneo ambayo wanaweza
kusaidia.
Post a Comment