Wajumbe
wa Mkutano wa 15 wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wenye asili ya Afrika ya
Kaskazini Magharibi ya Pacif Mjini Seattle wakijiorodhesha Tayari kwa
kuanza mkutano wao kwenye Hoteli ya Red Lion Mjini Settle.
Mwana Habari wa
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Othman Khamis akiwa katika
harakati za dondoo za kutafuta mambo mbali mbali kwa ajili ya kutuma
habari kwenye mkutano wa Chama cha wafanyabiashara wenye asili ya Afrika
Mjini Settle Nchini Marekani alipokuwa akizungumza na mmoja wa
wanajumuiya hiyo Bibi Darla Muya wa Marekani.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akilakiwa kwa ngoma katika mkutano
wa 15 wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wenye asili ya Bara la Afrika wa
Kaskazini Mashariki ya Pacific unaofanyika katika Hoteli ya Kimataifa ya
Red Lion kati kati ya Mji wa Seattlle Jimbo la Washington Nchini
Marekani.
Burudani katika mkutano
wa 15 wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wenye asili ya Bara la Afrika wa
Kaskazini Mashariki ya Pacific unaofanyika katika Hoteli ya Kimataifa ya
Red Lion kati kati ya Mji wa Seattlle Jimbo la Washington Nchini
Marekani.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akihutubia mkutano
wa 15 wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wenye asili ya Bara la Afrika wa
Kaskazini Mashariki ya Pacific unaofanyika katika Hoteli ya Kimataifa ya
Red Lion kati kati ya Mji wa Seattlle Jimbo la Washington Nchini
Marekani.
Wajumbe
toka Zanzibar wakibadilishana mawazo na mmoja wa wafanyabiashara
waliohudhuria mkutano wa 15 wa Jumuiya ya wafanyabiashara wenye asili ya
afrika Mjini Seattle.
Balozi
Seif Iddi na wajumbe wa mkutano wa 15 wa Jumuiya ya Wafanyabiashara
wenye asili ya Bara la Afrika wa Kaskazini Mashariki ya Pacific
unaofanyika katika Hoteli ya Kimataifa ya Red Lion kati kati ya Mji wa
Seattlle Jimbo la Washington Nchini Marekani. Wa pili kulia ni Afisa
Ubalozi Marekani, Bw Suleiman
Profesa
Margareth Kihara Mshauri wa masuala ya wajasiri amali Mjini Seattle
akizungumza na Mwenyekiti wa Chama cha wafanyabiashara wenye viwanda na
wakulima Zanzibar Abdulla Abass wakati wa mapumziko wa Mkutano wa 15 wa
Jumuiya ya wafanyabiashara wenya asili ya Afrika Mjini Settle. Kati kati yao ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha wafanyabiashara wenye viwanda na wakulima Zanzibar bwana Ali Aboud Mzee.
Mfanyabiashara wa chama cha wafanyabiashara kutoka Afrika Kusini Bwana Ndaba Cyril akifurahia
na kuridhika na vipeperushi vya mambo mbali mbali ya Zanzibar kwenye
meza ya Wafanyabiashara wa Zanzibar katika maonyesho yaliyokuwa nje ya
ukumbi wa Mikutano wa Red Lion ambao ulifanyika Mkutano wa 15 wa Jumuiya
ya wafanyabiashara wenye Assili ya Afrika Mjini Seattle.
Mwenyhekiti
wa chama cha Wafanyabiashara wenye viwanda na wakulima Zanzibar Abdull
Abass akimkabidhi zawadi maalum ya Picha inayoonyesha mandhari ya
Zanzibar iliyosarifiwa kwa majani ya Gomba Mjumbe wa Baraza la Mji wa
Seattle aliyemuwakilisha Meya wa Mji huo Bw. Bruce Harrel wakati wa
chakula cha mchana kwenye Mkutano wa Jumuiya ya wafanyabiashara wenye
asili ya Afrika Mjini Seattle. Picha zote na Hassan Issa wa OMPR.
-----------------------------------
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema wakati umefika
kwa Bara la Afrika kuhakikisha kwamba Mataifa yaliyomo ndani ya Bara
hilo yanajikita zaidi katika mfumo mpya wa uwekezaji badala ya ile
tabia ya mataifa hayo kuendelea kufanywa soko la bidhaa zinazotoka na
kuzalishwa nje ya Bara hilo.
Balozi
Seif alitoa kauli hiyo nzito kwenye mkutano wa 15 wa Jumuiya ya
Wafanyabiashara wenye asili ya Bara la Afrika wa Kaskazini Mashariki ya
Pacific unaofanyika katika Hoteli ya Kimataifa ya Red Lion kati kati ya
Mji wa Seattlle Jimbo la Washington Nchini Marekani.
Alisema
Bara la Afrika limebarikiwa kuwa na utajiri mkubwa wa mali asili,
rasilmali pamoja na vivutio kadhaa vya utalii ambazo vikitumika vyema
vinafursa ya kulipatia maendeleo makubwa na ya haraka bara hili
linaloendelea kukumbwa na umaskini na maradhi.
Balozi
Seif alifahamisha kwamba mkazo unapaswa kuchukuliwa na mataifa hayo
katika kuona miundo mbinu ya mawasiliano, usafiri, Utalii na hata makazi
yanaimarishwa ili kuongeza nguvu za uzalishaji sambamba na kuimarisha
uchumi kwa ustawi wa jamii za Bara la Afrika.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliupongeza Uongozi wa Jumuiya
ya Wafanyabiashara wenye asili ya Afrika ya Mjini Mjini Seattlle Nchini
Marekani kwa mipango yake iliyojipangia ya kusaidia nguvu za uzalishaji
kwa taasisi na vyama vya wafanyabiashara vya Nchi changa wakilenga zaidi
Barani Afrika.
Balozi
Seif aliwaomba wafanyabiashara wa Mji wa Seattle kupitia jumuiya yao
kufikiria kutoa upendeleo kwa Zanzibar katika kuwekeza kwa vile Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar imejitahidi kuimarisha miundo mbinu mbali
mbali kwa lengo la kutoa fursa bora kwa wawekezaji kuwekeza maeneo
tofauti ya Visiwa vya Unguja na Pemba.
Alifahamisha
kwamba zipo fukwe nzuri pamoja na viungo { Spice } vinavyotoa ushawishi
kwa wawekezaji wan je ya nchi kuhamasika kuwekea vitega uchumi vya
katika masuala ya Utalii.
“
Sera yetu ya uwekezaji iko wazi na inatoa fursa kwa wawekezaji wote iwe
wale wa taasisi na mashirika ya kigeni na hata wale wazalendo kuwekeza
katika maeneo tafauti hasa yale ya utalii ambayo Serikali yetu
imeyatilia mkazo zaidi katika kudaidia uchumi wake “. Alisisitiza Balozi
Seif.
Akigusia
maeneo mengine kama Kilimo, Viwanda Vidogo vidogo, mazao ya viungo
pamoja na Mawasiliano, Balozi Seif alisema milango iko wazi kwa
wawekezaji wa Marekani kutumia fursa hiyo ili kusaidia uchumi wa
Zanzibar sambamba na kuongeza ajira hasa kwa kundi kubwa la Vijana
wanaomaliza masomo yao wakiwa hawana kazi za kufanya.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar kupitia mkutano huo aliipongeza Serikali ya
Marekani kwa jitihada inazochukuwa za kuendelea kuiunga mkono Zanzibar
kwenye harakati zake za kujinasua kiuchumi na kujimarisha ustawi wa
Wananchi wake.
Alitolea
mfano wa mradi ya kataa malaria Zanzibar uliopunguza maradhi yazaidi ya
asilimia 80% ndani ya Visiwa vya Zanzibar, mradi wa umeme wa wats 100,
ujenzi wa bara bara zenye urefu wa kilomita 35 Kisiwani Pemba pamoja na
uimarishaji wa elimu ni miongoni mwa msaada mkubwa uliotolewa na Nchi
hiyo kwa Zanzibar.
Alieleza
kwamba maisha na harakati bora za kimaisha miongoni mwa wananchi wengi
wa Zanzibar imefanikiwa na kukua kutokana na miundo mbinu iliyowekwa na
Serikali kupitia washirika wa maendeleo yakiongozwa na lile la
changamoto ya millennia la Marekani { MCC }.
Naye
akitoa salamu za Chama cha wafanyabiashara, wenye viwanda na wakulima
Zanzibar Mwenyekiti wa Chama hicho Nd. Abdulla Abass aliwaeleza wajumbe
wa Mkutano huo wa Jumuiya ya wafanyabiashara wwenye asili ya Afrika
kwamba sekta ya bahari Kuu Zanzibar bado ina nafasi kubwa ya kuwekezwa
na wawekezaji wa Marekani.
Nd.
Abass alisema uvuvi wa Bahari kuu Zanzibar ambao unaweza kutoa ajira
kubwa kwa vijana pamoja na kuongeza mapato makubwa bado haujapata
uwekezaji katika kipindi kirefu.
Alisema
utafiti unaonyesha wazi kwamba Bahari inayovizunguuka Viziwa vya
Zanzibar bado ina utajiri mkubwa wa rasilmali inayoweza kunyanyua uchumi
na mapato ya Taifa.
Mapema
Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wenye asili ya Afrika Bwana Gishuru
Peter jumuiya hiyo ilyoanzishwa karibu miaka 16 iliyopita katika
mikakati yake ya baadaye imelenga kuvisaidia vyama na taasisi za
wafanyabiashara zipatazo 16 barani Afrika.
Bwana
Gishuru alisema hatua hiyo imepangwa ili kuziongezea nguvu jumuiya
mbali mbali Barani Afrika ziweze kujiendesha vyema kiuchumi na
kustawisha jamii zinazowazunguuka.
Hata
hivyo baadhi ya wataalamu waliopata fursa ya kutoa salamu na mada
kwenye mkutano huo wa 15 wa jumuiya ya wafanyabiashara wenye asili ya
Afrika ya Kaskazini Magharibi ya Pacific Mjini Seattle walisema Bara la
Afrika bado linaendelea kukumbwa na wimbi la idadi kubwa ya watu
wanaozaliwa bila ya mpango.
Mtaalamu
wa masuala ya takwimu kutooa chuo Kikuu cha Seattle Bwana Tonny Kelly
alisema ukanda wa Mataifa yaliyomo ndani ya jangwa la Sahara umekuwa
ukikabiliwa na ongezeko kubwa la idadi ya watu waliofikia asilimia 7.9%
hadi mwaka huu wa 2013.
Bwana
Tonny alisema kiwango hicho kikubwa kinatishia ustawi wa jamii zilizomo
ndani ya ukanda huo ambacho hakiendani sambamba na ukuaji wa uchumi wa
Mataifa hayo.
Mtaalamu
huyo wa masuala ya takwimu alifafanua kwamba zipo baadhi ya nchi za
Afrika zinaonyesha kupata mafanikio kiasi kutokana na mpango
ulioanzishwa wa pamoja wa Kibiashara kati ya Marekani na Afrika wa {
AGOA } ambao umetoa fursa kwa wafanyabiashara wa Mataifa kuuza bidhaa
zao Nchini Marekani kwa mpango maalum wa mashirikiano unaozingatia
unafuu wa ushuru kwa bidhaa hizo.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
9/11/2013.














Post a Comment