Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Chadema yashinda Unaibu Menya Arusha

KWA mara nyingine, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeibuka na ushindi wa nafasi ya Naibu Meya wa Jiji la Arusha. Katika uchaguzi huo uliofanyika jana mjini hapa, mgombea wa Chadema ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Daraja Mbili,Prosper Msofe alichaguliwa kwa kura 25 na kati ya hizo moja liharibika.


Jambo ambalo lilionekana kuwa na mvuto ni kitendo cha viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kushindwa kusimamisha mgombea katika nafasi hiyo.

Kutokana na hali hiyo, madiwani wa CCM na Chadema waliweka tofauti zao pembeni na kumchagua Msofe.

Akitangaza matokeo hayo, Meya wa Jiji la Arusha, Gaudenci Lyimo alisema uchaguzi ulifanyika kwa amani na kuwataka wote waliochaguliwa wafanye kazi.

“Nawaomba mno mfanye kazi maana ndiyo kazi mliyotumwa na wananchi wenu,”alisema Lyimo.


Alisema Diwani wa Kata ya Ngarenaro, Isaya Doita (Chadema), alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu na Afya.

Pia, alimtangaza Diwani wa Kata ya Moshono, Paul Patthsen (CCM) kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Miundombinu.

Kutokana na ushindi huo, wadau wa maendeleo walitafsiri kuwa huo ni mwisho wa msuguano baina ya CCM na Chadema ndani ya baraza la madiwani ambao umedumu muda mrefu na kukwamisha shughuli za maendeleo.

Kwa upande wake, Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha, Mary Chatanda alisisitiza kuwa katika uchaguzi huo chama hicho hakikutaka kusimamisha mgombea.

“Hatukutaka kusimamisha mgombea katika uchaguzi huu,lengo letu tulitaka wapinzani wapate nafasi ya uwakilishi katika baraza,” alisema Chatanda.

Alisema kwa kauli moja, CCM imebariki ushindi kwa sababu imechoka na malumbano yasiyokuwa na tija kwa wananchi.

Akionyesha furaha yake, Chatanda alimpongeza Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kwa kushiriki uchaguzi huo.

Alisema madiwani wa CCM watampatia ushirikiano Meya huyo.

Akizungumzia ushindi huo, Msofe alisema yuko tayari kushirikiana na Meya wa Jiji la Arusha,mkurugenzi na madiwani wenzake kuwaletea wananchi maendeleo.

“Kazi iliyo mbele yetu ni kuwaletea wananchi maendeleo, nitashirikiana na viongozi wote wa Halmashauri ya Jiji la Arusha,”alisema Msofe.

RAI
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top