Viongozi
wa Umoja wa Wafugaji wa Wilayani Nkasi wakionyesha hundi yenye thamani
ya shilingi milioni nane waliyopewa na COSTECH kama "Seed Fund" kwa
ajili kuendeleza kongano la wafugaji Wilayani humo. Kulia wanaoshuhudia
ni Ndugu Festo Maro Afsa Utafiti Mkuu wa COSTECH na Mkuu wa Mkoa wa
Rukwa Injinia Stella Manyanya.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na Wanakongano wa
Umoja wa Wafugaji wa Wilayani Nkasi (hawako pichani) katika Mkutano
uliofanyika Kalambo Ranch Wilayani humo tarehe 14 Novemba 2013. Mkuu
huyo Mkoa aliwataka wafugaji kufuga kisasa bila kuathiri mazingira kwa
kufuga mifugo michache inayoendana na maeneo husika, aliwataka pia
wafugaji kuwaendeleza watoto wao kielimu tofauti na ilivyo hivi sasa
amabao wengi wao hufanyishwa kazi za uchungaji wa mifugo. Katika hotuba
yake fupi alitoa agizo kwa halmashauri zote Mkoani Rukwa kuweka
kipaombele katika kutenga maeneo kwa ajili ya wafugaji na wakulima
katika kila kijiji na kujiwekea mkakati wa idadi ya mifugo itakayofugwa
kulingana na ukubwa wa eneo la malisho.
Ndugu
Festo Maro Afsa Utafiti Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia Nchini
COSTECH akizungumza na wanakongano wa Umoja wa Wafugaji wa Wilayani
Nkasi Mkoani Rukwa jana tarehe 14 Novemba 2013. Katika maelezo yake
alisema kuwa sio kila Kongano hupewa fedha za kianzio bali
hushindanishwa na kwamba Kongano la Umoja wa Wafugaji wa Wilayani Nkasi
likiwa na wanachama 167 limeibuka washindi kwa kuwa na mipango thabiti
ya kuendeleza shughuli zao za ufugaji kisasa kwa kuwainua kiuchumi,
kielimu, kiafya na kubwa zaidi bila kuathiri mazingira. Alisema Lengo la
COSTECH kutoa misaada kama hiyo ni kuwawezesha wadau wafanye shughuli
zao kisayansi zaidi.
Mkuu
wa Wilaya ya Nkasi Iddi Kimanta akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Rukwa
aweze kuzungumza na Wanakongano wa Umoja wa Wafugaji wa Wilayani humo
ambao yeye ndie muasisi wa umoja huo. Katika neno lake la awali
alimtaarifu Mkuu huyo wa Mkoa kuwa Umoja huo ulianzishwa mwaka jana 2012
tarehe 29 Agosti na kusajiliwa rasmi tarehe 30 Agosti 2013 ukiwa na
wanachama 167 na lengo kuu likiwa ufugaji bora wa kisasa usioathiri
mazingira na utakaomnufaisha mfugaji.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akimkabidhi Kaimu Mwenyekiti
wa Umoja wa Wafugaji wa Wilayani Nkasi Ndugu Pancras Maliyatabu Cheti
rasmi cha usajili wa umoja huo uliosajiliwa rasmi tarehe 30 Agosti
2013. Katikati anaeshuhudia ni Katibu wa umoja huo ndugu Jisena Biliya.
Picha ya pamoja.Picha na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa
Post a Comment