Msemaji wa hospitali hiyo, Tembogo Nyembezi, alithibitisha kuwa Dk Mgimwa alilazwa katika hospitali hiyo na sasa amesharuhusiwa.
Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Saada Mkuya, pia alithibitisha taarifa hizo .
"Ni kweli kwamba Dk Mgimwa alikuwa Afrika Kusini alikokuwa akitibiwa lakini hali yake inaendelea vyema. Ni maradhi ya kawaida ambayo yanaweza kumpata mtu yeyote lakini hajambo," alisema Mkuya.(P.T)
Mkuya alisema hali ya Dk Mgimwa ni nzuri na hakuna haja ya Watanzania kuwa na wasiwasi wowote.
Hata hivyo, Waziri Mkuya hakutaka kuweka wazi maradhi yanayomsumbua mkubwa wake.
Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi alisema hana taarifa za Waziri Mgimwa kuumwa na kwamba anachokifahamu ni kuwa mara ya mwisho alikuwa Washington kuhudhuria mkutano.
"Sasa kama aliugua ghafla sielewi. Mimi ni mnadhimu tu bungeni," alisema.

Post a Comment