Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akisimikwa usultani na mzee wa
kimila Alli Hassan Omar Linyama mara baada ya kuwasili katika kata ya
Nakapanya Wilayani Tunduru jana.
Sultan
Linyama Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi katika kata ya
Nakapanya Wilayani Tunduru Mkoa wa Ruvuma jana mara baada ya kuwasili
katika kata hiyo akitokea Wilayani Masasi Mkoani Mtwara katika ziara
yake ya kikazi ya siku 23 kwenye mikoa ya Ruvuma. Mbeya na Njombe
akikagua miradi mbalimbali na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama
cha Mapinduzi CCM na kuhamasisha wananchi katika suala zima la kushiriki
katika shughuli za maendeleo, Tatizo kubwa la mikoa ya Kusini hasa
Mtwara, Lindi na Ruvuma ni kuhusu bei ya zao la korosho ambapo Katibu
Mkuu Kinana amesisitiza kuwa Chama cha Mapinduzi kitahakikisha suala
hilo linashughulikiwa kwa umakini na Serikali ikishirikiana na taasisi
zinazohusika na zao hilo ili kukomboa uchumi wa wananchi wa eneo hilo
hasa kwa kuhakikisha viwanda vya kubangua korosho vinajengwa na vile
ambavyo vilibinafsishwa na havifanyi kazi kunaandaliwa utaratibu ambao
utawafanya waekezaji wengine kupewa ili vifanye kazi na kutatua tatizo
la bei ndogo ya zao hilo inayolipwa na wanunuzi wa korosho
zisizobanguliwa,Katika ziara hiyo Kinana ameongoza na Nape Nnauye
Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi na Dr. AshaRose Migiro Katibu wa
NEC Siasa na Uhusiano wa Kiamtaifa (PICHA NA KIKOSI KAZI CHA
FULLSHANGWE-TUNDURU)
Post a Comment