Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

KINANA ALIA NA WATENDAJI WA VYAMA VYA MSINGI VYA USHIRIKA NA BAADHI YA WATENDAJI WA SERIKALI MKOANI RUVUMA

 

 
1
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na Vita Kawawa Mbunge wa jimbo la Namtumbo Wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma mara baada ya kumpokea kwenye kata ya Mchomoro, Abdulrahman Kinana yuko katika ziara ya kikazi ya mikoa ya Ruvuma, Mbeya na Njombe ambapo ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi Ndugu Nape Nnauye na Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wakikagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzina kusikiliza matatizo ya wananchi ikiwa ni pamoja na kuhimiza wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo, Katika ziara hiyo ya Wilaya za Tunduru na Namtumbo wananchi wamelalamikia kuhusu bei  ya zao la Korosho ikiwa ni pamoja na Tumbaku, lakini pia wakalalamikia suala zima la Mbolea, ambapo Mbunge wa jimbo la Namtumbo Vita Kawawa  ametuhumu baadhi ya viongozi wa vyama vya ushirika na ofisa ushirika wa mkoa huo kuwabambikizia madeni wakulima wa tumbaku kupitia ruzuku ya mbolea  ambapo makadirio ya mbolea inayohitajika kwa wakulima huongezwa kinyemela na wananchi kuachiwa mzigo wa kulipa madeni ambayo hayawahusu jambo ambalo linawatesa wakulima wa tumbaku na kuwaacha wakiwa hoi kiuchumi (PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-NAMTUMBO) 3
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wa tatu kutoka kulia akipata kifungua kinywa nyumbani kwa mwenyekiti wa shina ndugu Hussein Rwambo wa pili kutoka kulia  katika kata ya Mchomoro, kulia ni Vita Kawawa Mbunge wa Jimbo la Namtumbo, Kushoto aliyekaa ni Dr. Asga Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa na aliyesimama mlangoni ni Nape Nnauye  Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi. 4
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kushoto ,  Vita Kawawa Mbunge wa Jimbo la Namtumbo kulia na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho wakichanganya Udongo wakati wakishiriki katika ujenzi wa Wodi ya wazazi katika hospitali ya wilaya ya Namtumbo ambayo inajengwa.
5
Kutoka kulia ni Vita Kawawa Mbunge wa Jimbo la Namtumbo, Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa Itikadi na Uenezi, Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Dr. Asha Rose Migiro wakishiriki katika ujenzi wa msingi wa wodi ya wazazi katika hospitali ya wilaya ya Namtumbo. 6
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kushiriki ujenzi wa msingi wa wodi ya wazazi katika hospitali ya wilaya ya Namtumbo. 7
Hili ni jengo la Utawala la hospitali ya Wilaya Namtumbo. 8
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na Vita Kawawa Mbunge wa jimbo la Namtumbo wakati alipokuwa akikagua majengo ya hospitali hiyo. 9
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Ndugu Said Mwambungu mara baada ya kukagua mtambo wa kuteketeza takataka na kuchemsha maji katika hospitali hiyo. 10
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata taarifa ya mtambo wa kufua umeme katika kituo cha kufua umeme cha Namtumbo. 11
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua jenereta na mtambo huo. 13
Kikundi cha ngoma kikitumbuiza  katika katika moja ya mikutano. 15
Mmoja wa wananchi akitoa kero za wakulima wa zao la Tumbaku kwa niaba ya wananchi. 16
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipiga picha ya pamoja na watumishi wa kituo cha kufua umeme mjini Namtumbo. 17
Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Taifa mjini Namtumbo leo. 18
Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa Itikadi na Uenezi akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa taifa mjini Namtumbo leo. 19
Wazee wa kimlia wakimvisha mgolole Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kama ishara ya heshima kwake kutokana na utendaji kazi uliotukuka katika chama. 20
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akiwahutubia wananchi mjini Namtumbo kwenye uwanja wa Taifa leo. 21
Mbunge wa Jimbo la Namtumbo Mh. Vita Kawawa akiwahutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara mjini Namtumbo, mkutano huo umefanyika kwenye uwanja wa Taifa.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top