Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (pichani) ameomba Bunge kuingilia
kati kuchunguza na kuwafikisha katika vyombo vya sheria, watu
waliotengeneza picha zinazomkashifu na kuzisambaza kwenye mitandao
mbalimbali ya jamii.
Akizungumza mjini hapa jana, Lema alisema picha hizo zimeanza kusambazwa tangu mwezi uliopita kwenye Mtandao wa Fikra Huru.
“Tayari nimemwonyesha picha hizi Spika Anne
Makinda na Katibu wa Bunge, wakanielekeza niandike barua uchunguzi uanze
na nimeandika barua tangu Novemba 11,” alisema Lema na kuongeza:
“Binafsi nina watu wangu, tumefuatilia na kubaini
wanaoendesha mchezo huu ni baadhi ya vijana wa Jumuiya ya Vijana CCM
(UVCCM), akiwamo mwenyekiti wake, Sadifa Juma Hamis na kada wa chama
hicho, Mtela Mwampamba.”
Hata hivyo, Mwampamba alimshangaa Lema kumhusisha na utengenezaji picha hizo na kumshauri kwenda mahakamani kama ana ushahidi.
“Namwambia aache woga, kila siku anapohubiri
hakuna dhambi kubwa kama woga, sasa kwa nini anakuwa mwoga, Lema
afanye siasa zenye tija mbona anajiita kamanda, kamanda gani anakuwa
mwoga aende mahakamani,” alisema.
Naye Sadifa alikanusha kuhusika na utengezaji wa
picha hizo na kwamba, hana sababu ya kufanya hivyo kwani hana tatizo
lolote na Lema.
“Natokea Zanzibar, yeye anatoka Arusha sasa kwa
nini nifanye hivyo wakati sina tatizo lolote na yeye, hili suala
lenyewe ndiyo nalisikia leo,” alisema Sadifa na kuongeza:
Lema alidai mwenyekiti huyo alikuwa akisambaza
picha hizo bungeni, akiwaonyesha wabunge mbalimbali hatua ambayo
ilimsababisha kupeleka malalamiko kwa Katibu wa Bunge na Spika.
Alisema alitaka kumvamia Sadifa akiwa bungeni
kumpokonya simu yake aliyokuwa akitumia kusambaza picha hizo, lakini
alizuiwa na Spika na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe.
MWANANCHI
MWANANCHI
Post a Comment