Makamu
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Philip Mangula akifurahia
jambo na Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima mara
baada ya kuwasili Mkoani Rukwa akitokea Katavi kwa ziara ya kichama hivi
karibuni. Mheshimiwa Mangula atamaliza ziara yake leo tarehe 12 Novemba
2013 Mkoani Rukwa ambapo amefanya mikutano mbalimbali ya nje na ya
ndani pamoja na kukagua miradi mbalimbali inayoendeshwa na Chama cha
Mapinduzi na Serikali.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Philip Mangula akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Kimanta alipowasili Wilayani hapo hivi karibuni kwa ziara ya kichama ya siku nne Mkoani Rukwa.
Makamu
Mwenyekiti wa CCM Philip Mangula akipeana mikono na Mbunge wa Nkasi
Kusini Ali Kessy maarufu kama Ali Mabodi katika ziara yake Wilayani
Nkasi hivi karibuni.
Makamu
Mwenyekiti wa CCM Taifa watatu kushoto, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Rukwa
Hiporatus Matete wa pili kushoto na Katibu wa CCM Mkoa wa rukwa
wakifurahia mapokezi ya wananchi wa kijiji cha Kizi kilichopo Wilayani
Nkasi waliokuwa wakimlaki Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa Ndugu Philip
Mangula kwa ujio wake Mkoani Rukwa.
Mkuu
wa Mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Mtumwa Rutengwe wa pili kushoto na msafara
wa viongozi wa Chama Tawala kutoka Mkoa wa Katavi wakiondoka katika
viwanja vya Kizi baada ya kumuaga na kumkabidhi Makamu Mwenyekiti wa CCM
Philip Mangula kwa viongozi wa Chama na Serikali Mkoa wa Rukwa kwa
ajili ya ziara ya kichama Mkoani humo.
(Na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)
Post a Comment