Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Rukwa Hiporatus Matete wapili kushoto kwa niaba ya
viongozi wa chama na Serikali Mkoa wa Rukwa akimuombea dua Makamu
Mwenyekiti wa CCM Taifa Ndugu Philip Mangula wakwanza kushoto aweze
kusafiri salama kuelekea Mkoani Mbeya katika maagano yaliyofanyika
Mpakani mwa Mkoa wa Rukwa na Mbeya tarehe 13 Novemba 2013. Wa kwanza
kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya.
Makamu
Mwenyekiti wa CCM Taifa Ndugu Philip Mangula akionyesha mchoro wa asili
wa Twiga aliopewa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya wa
pili kushoto katika hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na Mkuu
huyo wa Mkoa tarehe 12 Novemba 2013 kama ishara ya kulinda na kuzipenda
maliasili za taifa na kuendeleza vita dhidi ya ujangili nchini. Wa
kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Rukwa Ndugu Hiporatus Matete
na wa kwanza kulia ni Katibu wa CCM Mkoa huo Bi. Rahel Ndengeleke.
Mhe.
Mangula amesema amejifunza mengi Mkoani Rukwa ikiwemo mipango
mbalimbali ya maendeleo ya Chama na Serikali, alipendezewa na maendeleo
aliyoyaona sasa Mkoani Rukwa tofauti na miaka 10 iliyopita alipofika
Mkoani hapo kwa mara ya mwisho. Alifurahishwa na Mpango wa Serikali ya
Mkoa wa Rukwa wa ONYARU; Ondoa nyasi Rukwa ambao umehamasisha wananchi
wengi kuondoa nyasi na kuezeka bati katika nyumba zao.
Baadhi
ya viongozi wa chama (CCM) na Serikali Mkoani Rukwa wakiwa katika hafla
ya chakula cha jioni cha kuagana na Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa
Ndugu Philip Mangula katika Hoteli ya Holland Mjini Sumbawanga tarehe 12
Novemba 2013.
Baadhi
ya viongozi wa chama (CCM) na Serikali Mkoani Rukwa wakiwa katika hafla
ya chakula cha jioni cha kuagana na Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa
Ndugu Philip Mangula katika Hoteli ya Holland Mjini Sumbawanga tarehe 12
Novemba 2013.
Gari
anayoitumia Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa Ndugu Philip
Mangula ikitembea katika barabara ya Lami kutoka Sumbawanga kwenda
Jijini Mbeya. Sehemu kubwa ya Barabara hiyo kwa sasa imeshakalika
hususani miradi miwili ya Tunduma – Ikana na Ikana – Laela, mradi mmoja
wa Laela-Sumbawanga unaojengwa na Mkandarasi Aasleaff Bam International
ambao ulikua unasusua sasa unaendelea kwa kiwango cha
kuridhisha. Maendeleo haya ya barabara na mengine mengi aliyoyaona
yalikua kivutio kikubwa kwa Mhe. Mangula ambae alitoa ushuhuda kwamba
tangu afike Mkoani Rukwa mara ya mwisho mwaka 2003 na sasa hali ni
tofauti kabisa na kwamba kwa kipindi hicho cha Miaka 10 ameioana Rukwa
Mpya.
(Picha na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)
Post a Comment