Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MTOTO ATESEKA NA GONJWA LA AJABU

Na Imelda Mtema
WAKATI mamilioni ya watoto duniani wanafurahi kutokana na wazazi wao kuwa na uwezo wa kuwapeleka shule, sambamba na afya zao kuwa nzuri, hali ni tofauti kabisa kwa mtoto Hamisi Hashimu, mkazi wa Yombo Buza jijini Dar es Salaam ambaye kwa zaidi ya miaka sita sasa, yupo katika mateso makubwa.

Mtoto Hamisi Hashimu.
Hamis mwenye umri wa miaka 12, aliyezaliwa akiwa mzima wa afya, alipata ulemavu ghafla wakati akicheza na watoto wenzake, lakini jitihada za wazazi wake kumpeleka hospitali ya CCBRT ziligonga mwamba baada ya maradhi yake ya kuvimba mguu kushindwa kutibika na hivyo kulazimika kumrudisha nyumbani ambako hakwenda tena kutibiwa.
Akizungumza kwa uchungu, kijana huyo alisema anakumbuka siku moja akiwa mdogo alikuwa anacheza na wenzake ndipo miguu yake ilipovunjika kwa zaidi ya miaka sita sasa, mguu wake unaongezeka ukubwa kutokana na kuvimba, kitu kinachomfanya ashindwe kabisa kutembea.
“Mimi mpaka sasa hivi naendelea kuteseka kwa sababu wazazi wangu hawana uwezo kabisa wa kunisaidia kuhangaikia matibabu, kila siku mguu unaendelea kuwa mkubwa,” alisema Hamis.

Lakini katika hali ya kusikitisha zaidi, licha ya ulemavu huo unaompatia maumivu makubwa, bado Hamisi hulazimika kwenda Kariakoo kwa ajili ya kuomba hela kwa wasamaria wema mwishoni mwa wiki ili aweze kujikimu yeye na familia yao ambayo ni maskini.

“Huwa ninaenda shuleni kwa msaada wa kusukumwa kwenye baiskeli, siku za Jumamosi na Jumapili ndiyo huelekea Kariakoo kwa ajili ya kuomba msaada. Huu mguu ni mkubwa sana lakini kwa vile nina shida ndiyo maana najikokota ili niweze kupata fedha ya kujikimu katika maisha yangu ya kila siku,” alisema Hamisi.   

Kama umeguswa na habari za mtoto huyu na unapenda kumsaidia, wasiliana na chumba chetu cha habari kupitia namba 0713612533.

                GPL
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top